KLABU ya Manchester City imeisaidia Real Madrid kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester United kwa kuwapa Uwanja wa Etihad wafanyie mazoezi.
Jose Mourinho hakutaka kuutumia Uwanja wa Old Trafford kwa sababu una pitch mbaya na sasa watatumia Uwanja wa City.
Kutokana na matatizo ya ratiba za ndege kutoka Hispania, kocha huyo wa Real na timu yake hawatapata fursa ya kufanya mazoezi nyumbani Jumatatu kwa sababu ya kuwahi.
Mkono wa msaada: Timu ya Roberto Mancini imeipa Uwanja wa mazoezi Madrid kabla ya kuvaana na timu ya Sir Alex Ferguson.
Uwanja wa mechi, Old Trafford, umekataliwa na Mourinho kwa mazoezi
Jose Mourinho