MATAIFA 203 kutoka kila kona ya Dunia yako njiani kuelekea Rio de Janeiro, kati ya mataifa hayo ni mataifa 32 tu ambayo yatafika Brazil mwakani kwenye Kombe la Dunia.
Mataifa haya kidogo kidogo yaliingia kwenye soka la kimataifa kwenye ule mfumo wa mwenye nguvu ndiyo ataishi.
Kuna baadhi ya Mabara tunajua mataifa gani yataenda Brazil, lakini kwingine bado ni giza tupu.
Wakati tukielekea kwenye mwisho wa wiki ya heka heka za kufuzu, BIN ZUBEIRY tanakuletea kile ambacho kinaweza kutokea na wale wale wanaoweza kushiriki Kumbe la Dunia 2014.
Tunatamani mngekuwepo? Copacabana inawaita wachezaji bora duniani
ULAYA
Washindi wa makundi tisa watafuzu moja kwa moja kushiriki michuano ya mwakani. Washindi wa pili kwenye makundi (kwa kuangalia rekodi zao dhidi ya timu ya kwanza, tatu, nne, na ya Tano kwa sababu makundi mengine yanatimu chache) watafuzu baada ya kucheza mechi za mtoano.
Kundi A
Kuongoza Kundi: Ubelgiji
Nafasi ya pili: Croatia
Watakaokosa: Serbia, Macedonia, Wales, Scotland
Mechi muhimu: Croatia v Ubelgiji – Zagreb, Oktoba 11
Baada ya mechi nne kuchezwa, Ubelgiji na Croatia wanaonekana kuwa ndio vinara wa Kundi A.
Ubelgiji wanawachezaji kibao wenye vipaji, na mchango wa Eden Hazard, Thomas Vermaelen, Vincent Kompany na wanzao imesaidia kupata ushindi dhidi ya Wales, Scotland na Serbia.
Kazini: Nyota wa Chelsea, Eden Hazard akiichezea nchi yake, Croatia dhidi ya Ubelgiji, waliotoka nao sare ya 1-1 Septemba
Croatia nao wako vizuri na mechi kati yao iliyochezwa Brussels Septemba mwaka jana ilimalizika kwa sare ya bao 1-1. Mechi ya marudiano Oktoba 11 inaonekana ndiyo itaamua mshindi wa kundi.
Wales (wanapointi tatu) na Scotland (mbili) tayari timu hizi zinaonekana kukosa dalili za kushiriki Kombe la Dunia. Licha Gareth Bale kuwa mfungaji bora, lakini timu hiyo imepata vipigo kutoka kwa Ubelgiji na kichapo cha aibu cha mabao 6-1 kutoka kwa Serbia.
Sherehekea: Gareth Bale alifunga bao la ushindi dhidi ya Scotland, lakini Wales kwenda Brazil ni ndoto
Ushindi wa bao la Bale, ulirudisha heshima ya Wales dhidi ya Scotland Oktoba mwaka jana, lakini ushindi wao ulizimwa fasta na Croatia.
Scotland wao wanatamani kurudi kwenye michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo mwaka 1998. Lakini suluhu dhidi ya Serbia ilifuatiwa na sare ya bao 1-1 dhidi Macedonia.
Kundi B
Kuongoza kundi: Italia
Nafasi ya pili: Jamhuri ya Czech au Denmark
Watakaokosa: Bulgaria, Armenia, Malta
Mechi muhimu: Denmark v Italy – Copenhagen, Oktoba 11 – na Bulgaria v Jamhuri ya Czech – Sofia, Oktoba 15
Italia, tayari wanapointi 10 kwenye mechi nne walizocheza, tayari wanaonekana kufuzu. Walitoka sare na Bulgaria kwenye mechi ya kwanza, lakini tangu hapo wameshinda dhidi ya Malta na Armenia, pamoja na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Denmark, iliwapa utawala.
Muhusika: Mario Balotelli akisherekea baada ya kufunga bao la tatu la Italia dhidi ya Denmark, San Siro, Oktoba mwaka jana.
Chini yao kuna Bulgaria, Denmark na Jamhuri ya Czech ambao wote wanawania nafasi ya kucheza mechi za mtoano, huku wakiwa na uwezekano mkubwa sana wa kupolama pointi na kumuongezea faida Italia.
Kundi C
Kuongoza Kundi: Ujerumani
Nafasi ya pili: Sweden or Jamhuri ya Ireland
Watakaokosa: Austria, Kazakhstan, Faroe Islands
Mechi muhimu: Jamhuri ya Ireland v Sweden - Dublin, Septemba 6
Ujerumani wameshiriki kila Kombe la Dunia tangu mwaka 1950, wanaonekana wako njiani kwenda kwenye michuano hiyo mwakani licha ya kuruhusu Sweden kuchomoa mabao manne Oktoba 2012.
Inavutia: Sweden, walihamasishwa na Zlatan Ibrahimovic, kuchomoa mabao manne dhidi ya Ujerumani Oktoba mwaka jana.
Lakini kufuzu kwenda Brazil itakuwa siyo ngumu kwa Joachim Lowe kutokana na kikosi chake kujaa vipaji watu kama Bastian Schweinsteiger, Philipp Lahm na Mesut Ozil, itakuwa moja ya timu ambazo zitapewa nafasi ya kuchukua taji hilo.
Sita: Toni Kroos akifunga bao la Sita la Ujerumani waliposhinda 6-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland, jijini Dublin
Sweden, watakuwa nyumbani kesho kucheza na Ireland, lakini itakuwa mechi ya Septemba mwaka ambayo itaamua nani anakamata nafasi ya pili kwenye kundi lao.
Kundi D
Kuongoza kundi: Uholanzi
Nafasi ya pili: Hungary au Romania
Watakaokosa: Uturuki, Estonia, Andorra
Mechi muhimu: Romania v Hungary – Bucharest, Septemba 6
Timu ambayo iko vizuri kuliko Ujerumani kwa sasa ni Uholanzi ni ambao wameshinda mechi zao zote za kufuzu wakiwa wameshinda mabao 13 katika mechi zao nne. Tofauti kati yao na wengine ineonekana kutokana na ushindi wa mabao 4-1 iliyoupata dhidi ya washindi wa pili wa kundi hilo Hungary.
Inauma: Robin van Persie akichezewa faulo na Roland Juhasz wa Hungary, Uholanzi walishinda 4-1 jijini Budapest
Kundi E
Kuongoza kundi: Uswisi au Norway
Mshindi wa pili: Uswisi au Norway
Watakaokosa: Albania, Iceland, Slovenia au Cyprus
Mechi muhimu: Norway v Switzerland – Oslo, Septemba 10
Siyo kundi lenye msisimko sana, lakini moja ya kundi ambalo linaweza kuwahakikishia nafasi Norway kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo mwaka 1998. Hawakuanza vizuri walifungwa 2-0 na Iceland, lakini walizinduka na sasa wanakamata nafasi ya pili.
Wako England: wachezaji wa Norway, Erik Huseklepp (kulia), ambaye alicheza Portsmouth na Birmingham msimu uliopita akisherekea na kiungo wa Blackburn, Morten Gamst Pedersen
Lakini ni Uswisi ambao wanaonekana kupani kufika Brazil kwenye kundi hili, wemeshinda mechi dhidi ya Iceland na Slovenia, ambao wanaweza kutoa upinzani. Wemepoteza pointi walipopata sare ya bao 1-1 na Norway, Oktoba.
Group F
Kuongoza Kundi: Urusi
Mshindi wa pili: Israel au Ureno
Watakaokosa: Northern Ireland, Azerbaijan, Luxembourg
Mechi muhimu: Ureno v Israel – Lisbon, Oktoba 11
Wakiwa na Cristiano Ronaldo Ureno wangeweza kuonekana kama timu bora ya kundi huku wakifunga mabao mengi lakini mambo yamekwenda mrama.
Walipata ushindi mwembamba dhidi ya Luxembourg, kabla ya kufungwa na Urusi ambao kwenye kundi hili wanaonekana hawtaki mchezo kutokana na kushinda mechi zao zote nne za kwanza.
Bonge la Nyota: Nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo wanakazi ya kufanya kama wanataka kushiriki Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil
Kundi G
Kuongoza Kundi: Bosnia au Ugiriki
Mshindi wa Pili: Ugiriki au Slovakia
Watakaokosa: Lithuania, Latvia, Liechtenstein
Mechi muhimu: Bosnia v Ugiriki - Zenica, kesho
Bosnia wakipoteza nafasi hii kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza basi wasahau. Wakiwa na mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko akiongoza mashambulizi, wameanza kwa kasi mechi zao za kufuzu wakifunga mabao nane dhidi ya Liechtenstein, manne dhidi ya Latvia na matatu dhidi ya Lithuania.
Mwanzo: Edin Dzeko akiifungia Bosnia bao katika harakati zao za kusaka tiketi ya kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza
Kundi H
Kuongoza kundi: England
Mshindi wa pili: Montenegro au Poland
Watakaokosa: Moldova, Ukraine, San Marino
Mechi muhimu: England v Montenegro – Wembley, Jumanne – na England v Poland – Wembley, Oktoba 15
England wanakazi ya kufanya, katika mechi dhidi ya San Marino na Montenegro. Roy Hodgson atakuwa akitamani kukwepa kupitia kwenye mchujo katika harakati za kwenda Rio.
Kiwango: England wameshawafunga Brazil mwaka huu mabao ya Wayne Rooney na Frank Lampard
Kundi I
Kuongoza Kundi: Hispania au Ufaransa
Mshindi wa pili: Hispania au Ufaransa
Watakaokosa: Georgia, Belarus, Finland
Mechi muhimu: Ufaransa v Hispania – Paris, Jumanne
Hispania na Ufaransa watakuwa na bahati mbaya kutokana na kupangwa kundi moja, huku wakiwa na timu nyingine tatu za kujipigia.
Tangu mwanzo tulijua kwamba mechi kati yao itakuwa muhimu sana na ndiyo itaamua mshindi waa kundi hilo.
ASIA
Zinazoelekea kufuzu: Uzbekistan, Korea Kusini, Japan, Australia
Zinazopewa nafasi ndogo: Iran, Qatar, Iraq, Oman, Jordan
Mchuano mrefu wa bara la Asia kwa sasa hivi unaonekana kuanza kufunguka na timu zenye nafasi ya kufuzu zimeanza kuonekana.
Mechi zinacheza wikiendi hii na kukamilishwa Juni. Washindi wawili wa ju kwenye kila kundi wanaenda mija kwa moja, na washindi wa tatu wanashiriki hatua ya mtoano na washindi kutoka Amerika Kusini.
Njiani: Kiungo wa Japan na Man United, Shinji Kagawa akiwa kazini
KUNDI A
1. Uzbekistan Pld 5 GD +1 Pts 8
2. South Korea Pld 4 GD +5 Pts 7
3. Iran Pld 5 GD 0 Pts 7
4. Qatar Pld 5 GD -2 Pts 7
5. Lebanon Pld 5 GD -4 Pts 4
2. South Korea Pld 4 GD +5 Pts 7
3. Iran Pld 5 GD 0 Pts 7
4. Qatar Pld 5 GD -2 Pts 7
5. Lebanon Pld 5 GD -4 Pts 4
KUNDI B
1. Japan Pld 5 GD +11 Pts 13
2. Australia Pld 4 GD 0 Pts 5
3. Iraq Pld 5 GD -1 Pts 5
4. Oman Pld 5 GD -3 Pts 5
5. Jordan Pld 5 GD -7 Pts 4
2. Australia Pld 4 GD 0 Pts 5
3. Iraq Pld 5 GD -1 Pts 5
4. Oman Pld 5 GD -3 Pts 5
5. Jordan Pld 5 GD -7 Pts 4
Not this time: North Korea, who were the centre of attention in 2010, have been eliminated
Tuesday’s two fixtures – Uzbekistan v Lebanon and South Korea v Qatar – will help break the deadlock.
In Group B, Japan are odds-on to reach a fifth successive finals with four wins and a draw so far. Australia were the side to take points off them and should emerge ahead of Iraq, Oman and Jordan given their greater pedigree. Next week, Australia host Oman and Jordan play Japan.
AFRICA
Vinara wa makundi: Ethiopia, Tunisia, Ivory Coast, Zambia, Congo, Nigeria, Misri, Benin, Libya, Senegal
Utakuwa upuuzi kuanza kutabiri timu zitakazofuzu Afrika kwa sasa kwa sababu michuano yao bado iko kwenye hatua za awali kabisa, lakini tuwategemee timu miamba za bara hilo kushiriki tena.
Nigeria, mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika.
Ivory Coast wamejipanga vya kutosha kwenda Brazil
AMERIKA KASKAZINI NA KATI
Mashindano ya CONCACAF yako kwenye mzunguko wanne na wamwisho timu tatu za juu zinafuzu moja kwa moja kwenda Brazil.
Clint Dempsey akishangilia baada ya kuifungia Marekani bao
AMERIKA YA KASKAZINI
1. Honduras Pld 1 GD +1 Pts 3
2. Costa Rica Pld 1 GD 0 Pts 1
3. Panama Pld 1 GD 0 Pts 1
4. Jamaica Pld 1 GD 0 Pts 1
5. Mexico Pld 1 GD 0 Pts 1
6. United States Pld 1 GD -1 Pts 0
2. Costa Rica Pld 1 GD 0 Pts 1
3. Panama Pld 1 GD 0 Pts 1
4. Jamaica Pld 1 GD 0 Pts 1
5. Mexico Pld 1 GD 0 Pts 1
6. United States Pld 1 GD -1 Pts 0
Mexico and the States will be the obvious favourites to qualify, both having emerged from the previous group phase as winners. Having gained a taste in South Africa 2010, Honduras will be hoping for a return ticket, while Jamaica haven’t got there since France 1998. Panama would be first-time qualifiers.
On Friday, Honduras welcome Mexico, Jamaica play Panama and the US play Costa Rica in Colorado.
AMERIKA
Wakati huu ambao Brazil hawashiriki kwenye hatua ya kufuzu ugumu kwenye michuano ya Amerika Kusini umepungua Lionel Messi na jeshi lake ndio wanakimbiza kwenye bara hilo la soka.
Mfungaji Bora: Lionel Messi amefunga mabao saba akiwa na Argentina
KUNDI LA AMERIKA KUSINI
1. Argentina Pld 9 GD +13 Pts 20
2. Ecuador Pld 9 GD +3 Pts 17
3. Colombia Pld 9 GD +8 Pts 16
4. Venezuela Pld 9 GD -1 Pts 12
5. Uruguay Pld 9 GD -2 Pts 12
6. Chile Pld 9 GD -4 Pts 12
7. Bolivia Pld 9 GD -2 Pts 8
8. Peru Pld 9 GD -5 Pts 8
9. Paraguay Pld 9 GD -10 Pts 7
2. Ecuador Pld 9 GD +3 Pts 17
3. Colombia Pld 9 GD +8 Pts 16
4. Venezuela Pld 9 GD -1 Pts 12
5. Uruguay Pld 9 GD -2 Pts 12
6. Chile Pld 9 GD -4 Pts 12
7. Bolivia Pld 9 GD -2 Pts 8
8. Peru Pld 9 GD -5 Pts 8
9. Paraguay Pld 9 GD -10 Pts 7
Their only slip-up to date was a 1-0 defeat in Venezuela on matchday two, but impressively they have gained wins in Chile and Columbia along the way and have been very clinical at home.
Ecuador and Columbia are jostling beneath, while a real scrap is on the cards for the other places between Venezuela, Uruguay and Chile. Luis Suarez has been carrying his county’s hopes with seven strikes so far.
On Friday it’s Columbia v Bolivia, Uruguay v Paraguay, Argentina v Venezuela and Peru v Chile.
OCEANIA
Pande za Oceania, New Zealand kama kawaida wako vizuri kushiriki tena kwenye michuano ya mwakani nchini Brazil kutokana na kutawala soka la kwenye visiwa vya huko.
New Zealand hawakufungwa kwenye Kombe la Dunia 2010, Shane Smeltz akifunga dhidi ya Italia.