AKIWA bado mchezaji wa Manchester City inayopambana kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu England, beki Vincent Kompany ameamua kununua klabu inayosuasua katika Ligi Daraja la Tatu Ubelgiji, FC Bleid.
Ikiwa imeshinda mechi mbili tu katika ya 28 ilizocheza D3B msimu huu, klabu hiyo kutoka Jiji la Brussels iko mkiani mwa Ligi na ina deni la pointi 16 ili kuwa salama, lakini Kompany anaamua kuwekeza huku akiendelea kucheza.
Katika taarifa iliyobandikwa katika tofuti mpya ya klabu hiyo, WeStartFromScratch.com, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameelezea sababu zake za kuinunua timu hiyo kuwekeza ili irejeshe makali yake na kuwa tishio Ulaya.
Kombora: Kompany, anaonekana hapa akiwa na Mousa Dembele (kulia), hajawahi kuona aibu kuonyesha mapenzi yake kwa nchi yake.
Na Kompany anawakaribisha wadau wa soka, awe shabiki au asiwe shabiki wa klabu hiyo, kujitokeza kusaidia mawazo ya kupatikana kwa jina jipya la klabu hiyo.
Karibu: Kompany amemkaribisha yeyote kuchangia wazo la jina jipya la klabu
Kompany, ambaye amekulia Brussels, amesema: "Ni mchezo wangu na jukumu la kijamii la kuwaunganisha vijana wa Brussels.
Vijana wa Brussels, kutoka sehemu tofauti, wanang'ara na wanajiamini mno, lakini hawapewi nafasi.
"Mimi ni miongoni mwao na ninamini kwa jitihada hizi katika eneo sahihi, wanaweza chochote... kama watapewa nafasi,"alisema beki huyo.
Beki huyo hayuko peke yake katika uwekezaji huo, na anasema ataendelea kuzingatia ajira yake Eastlands na majukumu yake katika timu ya taifa ya Ubelgiji.
Furaha na timu ya taifa: Beki mzaliwa wa Brussels (chini kabisa) anataka kulipa fadhila nyumbani kwao kwa kuwekeza katika klabu