MSHAMBULIAJI Mario Balotelli alikuwa maarufu kwa vituko vyake na tabia za ajabu wakati akiwa Manchester City na anaonekana hajabadilika sana hata baada ya kurejea Italia.
Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Ghana, alikutwa amelala kwenye eneo la juu la kuwekea mizigo ndani ya pamoja na wachezaji wenzake M'Baye Niang na Stephan El Shaarawy.
El Shaarawy mwenye umri wa miaka 20, ambaye jina lake la utani ni 'Farao', amebandika picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter akiwa amelala eneo la kuwekea mizigo na wachezaji wenzake hao wa Milan.
Machizi: Mario Balotelli (kushoto), M'Baye Niang (kulia) na Stephan El Shaarawy wakiwa wamelala eneo la kuwekea mizigo wakati siti zipo wazi.
MILAN YAILAZA CHIEVO
Soma taarifa ya AC Milan kuichapa bao 1-0 Chievo juzi Jumamosi HAPA
Balotelli alijiunga na Milan January baada ya misimu miwili na nusu ya kufanya kazi Manchester na ameendelea kuwa maarufu tangu arudi nyumbani.
Mshambuliaji huyo alifunga mabao mawili dhidi ya Udinese na amefunga mabao matano katika mechi za Serie A tangu wakati huo.
Pia aliifungia mabao yote Italia wiki iliyopita ikishinda 2-0 katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Malta kabla hajaisaidia Milan kushinda 1-0 mbele ya Chievo Jumamosi na kuongeza matumaini ya timu yake kufuzu Ligi ya Mabingwa.
Nyota: Balotelli ameisaidia Milan kuifunga Chievo 1-0 katika mechi ya Serie A Jumamosi
Anapiga mabao tu: Mshambuliaji huyo amekuwa mwiba tangu arejee nyumbani
Anawakilisha taifa: Balotelli alifunga mabao yote wakati Italia ikishinda 2-0 dhidi ya Malta wiki iliyopiya
Balotelli katika mechi ambayo Italia iliifunga 2-0 Malta