Kabeya Badu |
Na Princess Asia
MWANAMUZIKI wa siku nyingi nchini, Kabeya Badu ambaye mara ya mwisho alikuwa na bendi ya Wazee Sugu amefariki dunia asubuhi ya dunia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya figo.
Kwa mujibu wa mwanamuziki mwingine mkongwe, John Kitime, figo za ma marehemu zilifikia kushindwa kufanya kazi.
Kifo cha Badu, siyo mtu pigo kwa bendi yake Wazee Sugu, bali kwa tasniya zima ya muziki nchini kwa ujumla.
Enzi za uhai wake, kabla ya Wazee Sugu, Badu alipigia bendi bendi mbalimbali zikiwemo Orchestra Fovette, Orchestra Safari Sound, Orchestra Marquis, Intimate Rhumba, Tancut Almasi na nyinginezo.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amyn.
Kabeya Badu akiwa na Kasongo Mpinda kulia enzi za uhai wake |