// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); FIRST ELEVEN AZAM NA WAJESHI WA LIBERIA HII HAPA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE FIRST ELEVEN AZAM NA WAJESHI WA LIBERIA HII HAPA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 17, 2013

    FIRST ELEVEN AZAM NA WAJESHI WA LIBERIA HII HAPA

    Mwadini kulia akimpongeza Kipre Tchetche baada ya kugunga bao dhidi ya Al Nasir. Wote wanaanza leo.

    Na Mahmoud Zubeiry
    KIPA Mwadini Ally ataendelea kusimama langoni Azam FC leo wakati ikimenyana na Barack Young Controllers kwenye Uwanja wa Antonette Tubman mjini Monrovia katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, itakayoanza saa 10:00 za Liberia sawa na saa 1:00 Tanzania.
    Kocha Muingereza wa Azam, Stewart Hall ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mbali na Mwadini kuanza langoni, beki wa kulia atakuwa Himid Mao, kushoto Waziri Salum, katikati David Mwantika na Joackins Atudo, wakati viungo watakuwa Ibrahim Mwaipopo chini, Humphrey Mieno juu, kulia Kipre Balou, kushoto Khamis Mcha ‘Vialli’ na washambuliaji John Bocco ‘Adebayor’ na Kipre Tcheche.
    Hall alisema katika benchi atakaa pamoja na Aishi Manula, Luckson Kakolaki, Malika Ndeule, Abdulhalim Humud, Jabir Aziz, Abdi Kassim ‘Babbi’ na Seif Abdallah.
    Wachezaji wengine walio na Azam Monrovia ni Uhuru Suleiman, Brian Umony na Gaudence Mwaikimba. Salum Abubakar ‘Sure Boy’ alibaki kutokana na kusumbuliwa na Malaria.
    Wawakilishi hao wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, wamelazimika kujilipia wenyewe hoteli mjini Monrovia kwa siku zote watakazokuwa nchini Liberia tangu Jumatano kwa ajili ya mchezo huo kufuatia kutoridhishwa na mazingira na hadhi ya hoteli.
    Barrack Young Controllers inayomilikiwa na jeshi la nchini humo, iliyoanzishwa mwaka 1997, inatumia Uwanja wa Antonette Tubman uliopo mjini Monrovia kwa mechi zake na haina tofauti sana na Azam kihistoria. 
    Wakati Azam ilianzishwa mwaka 2004 na kucheza Ligi Kuu ya nchi kwa mara ya kwanza mwaka 2008, hadi sasa ina mataji mawili ya Kombe la Mapinduzi na moja la Kombe la Hisani ya nchini DRC, wapinzani wao wana mataji mawili ya Kombe la Liberia na moja la Super Cup ya nchini humo.
    Azam ni timu pekee ya Tanzania iliyobaki kwenye michuano ya Afrika baada ya Simba na Jamhuri ya Pemba kutolewa katika Raundi ya Kwanza tu ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Azam inayomilikiwa na Alhaj Said Salim Awadh Bakhresa na faimili yakle, ilifuzu kuingia Raundi ya Pili ya michuano hiyo, baada ya kuichapa jumla ya mabao 8-1 Al Nasir Juba ya Sudan.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: FIRST ELEVEN AZAM NA WAJESHI WA LIBERIA HII HAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top