// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CAZORLA: SOKA YA ENGLAND ACHANA NAYO, HISPANIA UFUNDI ZAIDI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CAZORLA: SOKA YA ENGLAND ACHANA NAYO, HISPANIA UFUNDI ZAIDI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 02, 2013

    CAZORLA: SOKA YA ENGLAND ACHANA NAYO, HISPANIA UFUNDI ZAIDI

    SANTI Cazorla anakaribia. Ni mdundo wa mpira wa ngozi kwenye aridhi ambao unatoboa siri. Kelele za kabati la jirani na mlango unafunguka anaingia kijana mmoja mfupi akiwa amejawa tabasamu usoni.
    Cazorla ananikaribia na kunipa mkono, anaangusha mpira na unatua kwenye mguu wake wa kushoto – mguu usio na nguvu – anauacha umeganmda hapo unakaa hapo kwa sekunde kadhaa kabla hajaupiga juu na kucheza danadana kadhaa kabla ya kuushika mpira huo mkononi na kukuaa chini.
    Anamiaka 28, lakini ni wazi kwamba hii imekuwa staili yake anayopenda kuingilia. Nyumbani kwao kwenye mitaa ya Lugo de Llanera alikuwa kijana wa kawaida tu na mpira mkononi ambaye aliwahi kuonekana kwenye mara moja kwenye mkanda wa Michael Laudrup enzi hizo.

    Maestro: Arsenal's Santi Cazorla speaks in an exclusive interview with Sportsmail
    Maestro: Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla alifanya mahojiano maalumu na Sportsmail

    Sasa hivi ni staa ambaye anatawala kwenye baa za mji huo.
    “Nimejifunza soka langu mitaani, nikicheza shuleni, nilikuwa nikicheza mpira kwa masaa 24 katika siku saba za wiki,” alisema “Kuna wakati tulipokonywa mipira yetu, lakini tulitengeneza mwingine kwa kutumia soksi au kitu chochote kile ambacho tungekipata. Tulikuwa tukiadhibiwa kwa sababu tulitumia muda mwingi kucheza soka badala ya kwenda kusoma.
    “Nilikuwa nikiangalia kikosi bora cha Real Madrid, na Laudrup ndiye nilikuwa nampenda sana.
    “Nilikuwa naweza kucheza kwa kutumia miguu yote. Ilikuwa ni zawadi. Mazoezi yanasaidia, lakini nimekuwa nikifanya mambo makubwa tangu nikiwa mdogo. Huwa sitilii maanani mguu gani unakuwa imara zaidi, huwa nafanya mazoezi kawaida na ninatumia miguu yote miwili. Naweza kusema kwamba mimi natumia mguu wa kulia, nikipiga penalti napenda kupigia mguu wa kulia.”

    Double figures: Cazorla has scored 11 Premier League goals since his arrival in the summer
    Cazorla amefunga mabao 11 kwenye Ligi Kuu ya England msimu huu
    Double figures: Cazorla has scored 11 Premier League goals since his arrival in the summer
    Huo ndio uwezo wake ambao umewavutia mashabiki kwenye msimu wake wa kwanza akiwa na Arsenal. 
    Kama mchezaji binafsi, Cazorla anafanya mpira uonekane mchezo rahisi sana, hata kama The Gunners kama timu haijafanya hivyo, na anajua ni mabao mangapi amefunga kwenye Ligi Kuu ya England, “Mabao 11,” alisema “Rekodi yangu iliyopita ilikuwa mabao tisa nikiwa Malaga. Ni kitu (Kufunga mabao) ambacho kila siku nakifanyia kazi na mwaka huu nimeweza kupandisha uwezo wangu. Natumaini nitafunga mabao zaidi kabla ya msimu huu kuisha, kila mechi nitajaribu. Labda nitafikisha mabao 15.
    “Kulinganisha na Hispania, soka la hapa halina ufundi mwingi, lakini linavutia kucheza na kuangalia. Kunaufundi mwingi Hispania na wanabanwa na hili. Hili linafanya soka kukosa mvuto. Kuna kasi kubwa sana England.
    “Unapata nafasi sana uwanjani, hasa kwa mchezaji kama mimi, na unapata muda mwingi wa kufikiria. England timu zinataka kushambulia na kufunga mabao. Hispania watu wanabanwa na ufundi. Mazingira hapa yanavutia sana.”
    Itakuwa joto kesho pale Arsenal watakapofanya safari fupi kwenda kupambana na Tottenham, kwenye mechi kali ambayo itakuwa muhimu kwa timu zote mbili. Ushindi utaipaisha Arsenal na kuifanya kuwa na pointi moja nyuma ya majirani zao. Kufungwa inamaana wataachwa kwa pointi saba na watani wao wa jadi wa London Kaskazini.
    “Hii ni mechi muhimu sana kwetu hasa ukiangalia nafasi ya kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya,: alisema Cazorla, “Tukifungwa tofauti ya pointi kati yetu na wao itakuwa pointi saba, ni pengo kubwa sana hilo.
    “Ni kweli tumeshindwa kucheza kuwa kiwango cha juu kwenye mechi zote. Tumeshindwa kusonga mbele kwenye Kombe la Ligi au Kombe la FA, lakini tumedfhamiria kushiriki Ligi ya Mabingwa na tunatumaini tutafanya vizuri mpaka mwisho wa msimu. Ushindi kwa Tottenham utaipa moyo timu nzima. Tuko pointi mbili nyuma ya Chelsea, tukishinda mechi ya kesho tutakuwa pointi moja nyuma ya Tottenham.’

    Enjoying life: Cazorla says life in London is very different to Spain but he's loving it
    Anafurahia maisha: Cazorla anasema maisha ya London ni tofauti na Hispania lakini anayapenda.
    Cazorla ni mtoto wa mchimba madini kutoka Asturias, eneo lililopo Kaskazini mwa Hispania. Juan Mata na Michu pia wanatoka huko, na ni zao la Chuo cha soka cha Real Oviedo. Watatu hao wamenunua hisa kutoka kwenye klabu yao ya zamani ilikuisaidia isifilisike.
    “Soka la Asturias haliko kwenye kipindi chake bora, lakini siku zote limekuwa likizalisha wachezaji wazuri kwa timu nyingine za Hispania na duniani kwa ujumla,” Aliongeza Cazorla. 
    Baba yake Jose Manuel alikuwa kwa Ugonjwa wa Moyo miaka sita iliyopita akiwa na miaka 48, lakini mama yake Lolli na kaka yake Nando wanaishi Llanera.

    Honest: Cazorla admitted Arsenal have been inconsistent this season
    Afunguka: Cazorla amekiri kwamba Arsenal imekuwa na msimu mbaya 
    “Ni muhimu kwa kila mtu kujua wanatoka wapi,” alisema Cazolrla. “Hata kama wewe ni mchezaji unahaki sawa na watu wengine na hilo halitakiwi kubadilika kivyovyote.
    “Baba yangu alikuwa mchimba madini – baba yake David Villa naye alikuwa hivyo – baba za rafiki zangu wengi hiyo ni kazi yao. Ni kazi yenye hashima kubwa sana na ni ngumui pia. Sidhani kama ningeweza kuifanya. Nimekuwa napenda sana computers labda ningeangukia huko kama isingekuwa soka.”
    Kama Real Oviedo, sekta ya madini iko kwenye hali nzuri.
    Wachimbaji nmadini wa Asturia walifanya migomo kadhaa mwaka jana, walitembea hadi Madrid wakipinga mpango wa serikali wa kufunga migodi yao.

    Favourite: Cazorla used to watch Dane Michael Laudrup play for the Barcelona 'Dream Team'
    Kivutio chake: Cazorla alipenda kumuangalia Michael Laudrup akiwa na kikosi cha Real Madrid 

    ARSENE YUKO SAWA              

    Arsene Wenger ataiongoza timu yake kwenye north London derby ikiwa ni mara yake ya 40 kufanya hivyo huku akifungwa mara nne tu katika kipindi cha miaka 16 akiwa na Arsenal.
    Wenger ameshinda mara 18 na kutoka sare 17, lakini sasa hivi kuna mabadiliko sana hasa White Hart Lane. The Gunners hawajashinda mechi yoyote ya Ligi Kuu kwenye uwanja huo katika mechi nne za mwisho.
    Hii itakuwa mechi ya pili ya Andre Villas-Boas, akifungwa ya kwanza kwa mabao 5-2 Novemba mwaka jana kwenye uwanja wa Emirates. Pia alifungwa 5-3 na Arsenal alipokuwa kocha wa Chelsea, Oktoba 2011.
    “Wanatakla kufunga baadhi ya migodi na hilo litakuwa baya kwaa Asturias, hasa kutokana na kutegemea machimbo ya makaa yam awe,” alisema Cazorla. “Mambo hayako sawa kule kwa sasa, lakini natumaini hawatafunga. Watu wengi watapoteza kazi zao.”
    Mabadiliko yake tangu alipotua Arsenal kutoka Malaga yamekuwa safi. Cazorla amekuwa na matukio ya kufurahisha, lakini amekuwa akifurahia zaidi kuliko mara ya kwanza alipokutana na Arsenal. Il;ikuwa kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Aprili 2006 na alikuwa mchezaji kinda wa Villarreal ambaye aliuukosa mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi. Aliangalia mechi hiyo kutokea benchi katika uwanja wa El Madrigal wakati Yellow Submarine waliposhindwa kubadili matokeo ya bao 1-0 walilofungwa ugenini kwenye mechi ya kwanza.
    Walipopata penalti kwenye dakika ya 90, ilionekana kama Juan Roman Riquelme angepeleka pambano hilo kwenye muda wa nyongeza, lakini Jens Lehmann aliiokoa Arsenal na kuipeleka fainali dhidi ya  Barcelona jijini Paris.

    Painful memory: Jens Lehmann saved Juan Roman Riquelme's late penalty as Arsenal beat Villarreal in the Champions League semi-finals in 2006
    Maumivu: Jens Lehmann akiokoa penalti Juan Roman Riquelme mwaka 2006Painful memory: Jens Lehmann saved Juan Roman Riquelme's late penalty as Arsenal beat Villarreal in the Champions League semi-finals in 2006

    11 WA KWANZA LONDON KASKAZINI

    Jamie Redknapp alichagua kikosi chake bora cha North London DerbyHAPA
    “Kilikuwa kipindi kigumu kwa timu,” alisema Cazorla. “ilikuwa ni hatua moja kabla ya kufika fainali na tulisikitika kwa sababu tulikuwa na uhakika kwamba nafasi hii inaweza isije kujirudia. Timu ilitoka pale mpaka kushuka daraja msimu uliopita.
    “Lakini Riquelme ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani. Yuko kwenye kiwango kimoja na watgu kama kina Ronaldinho na Zinedine Zidane. Ni mmoja kati ya wachezaji bora zaidi niliowahi kucheza nao.
    “Sijafikia kiwango chake. Nilikuwa na bajati kucheza miaka miwili na Riquelme. Nilikuwa najifunza kila siku kwa kufanya nae mazoezi na kucheza nane. Ni mchezaji ambaye anaweza kuleta mabadiliko uwanjani. siwezi kusahau nafasi niliyopata kucheza na mchezaji kama yeye.”
    Hispania inaonekana kutawala soka la viungo mafundi duniani, ambao wanakuwa huru wakiwa na mpira mguuni, wanaweza kupita mabeki na kutoa pasi kwenye wakati muafaka.

    Praise: Cazorla described team-mate Jack Wilshere as 'an amazing player'
    Sifa: Cazorla anamtaja Jack Wilshere kama mchezaji wa kipekee
    “Kizazi cha wachezaji wa aina hii kimezaliwa Hispania ambako wanaangalia sana masuala ya ufundi,” alisema Cazorla, ambaye alishangaa sana kujua kwamba Jack Wilshere  ni Muingereza mwenye kiwango kam,a cha Wahispaniola ambaye amekulia Arsenal. “Ni mcheza wa kipekee. Alikuwa majeruhi nilipofika na sikuwa namjua sana, lakini kila mtu alikuwa akimsifia. Baada ya kumuona akicheza unaelewa kwa nini kila mtu anatarajia makubwa kutoka kwake.
    “Ni kijana mdogo ambaye atakuja kufanya makubwa siku za usoni. Ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Arsenal na Ligi Kuu ya England. Ni wazi atakuja kuwa mchezaji wa kiwango cha juu duniani, ni kama mchezaji wa Kihispania, anapogusa mpira na ufundi wake. Siyo kumiliki mpra tu lakini anajua jinsi ya kuutumia. Nadhani yuko kamaDavid Silva: anatumia mguu wa kushoto na anajua kupanda mbele na mpira.”
    Mchezaji mwingine wa Kiingereza ambaye amemvutia Cazorla ni Gareth Bale.

    Test: The Spaniard will come up against Gareth Bale in the north London derby on Sunday
    Jaribio: Cazorla atakutana uso kwa uso na Gareth Bale 
    “Bale ni mchezaji mzuri sana ni wazi yeye ndiye sehemu muhimu nya mechi ya kesho, pamoja na kuwa wanawachezaji wengi wazuri. Inawezekana akawa ndie bora England kwa sasa.” Alisema Cazorla
    “Ananikumbusha Cristiano Ronaldo. Wanafanana jinsi wanavyokimbia na jinsi wanavyopiga mashuti wote wananguvu sasa.

    VIDEO: MAHAJOJIANO MAALUM NA CAZORLA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: CAZORLA: SOKA YA ENGLAND ACHANA NAYO, HISPANIA UFUNDI ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top