ROMAN Abramovich ataangalia upya nafasi ya Rafa Benitez kama kocha wa muda wa Chelsea, baada ya mashabiki konyesha kutokumtaka kocha huyo baada ya mechi ya Jumamosi dhidi ya West Bromwich.
Benitez amewakera mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuwaponda dakika chache baada ya klabu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Middlesbrough na kujihakikishia nafasi ya kucheza nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester United.
Zaidi ya mashabiki 1,900, waliojitolea kusafiri kwa umbali wa Mile 500 kwenda kuishangilia timu yao walishangazwa na jinsi alivyowaponda, wakati wa mechi hiyo dhidi ya vibonde wa Ligi Daraja la Kwanza, na sasa asubiri kupata wakati mgumu dhidi ya Stamford Bridge.
Huruma: Benitez akiiongoza timu yake mazoezini jana, amekuwa na wakati mgumu kutoka kwa mashabiki tangu siku ya kwanza alivyofika kwenye klabu hiyo.
Abramovich tayari anaangalia machaguo yake baada ya Benitez kuitwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chelsea, Ron Gourlay kuzingumza juu ya matatizo ndani ya klabu hiyo.
Mmiliki wa klabu hiyo anakosa mtu muafaka atakayechukua majukumu ya kuinoa Chelsea kwa muda, lakini Jose Mourinho, ambaye alitosa kurejea klabuni hapo msimu uliopita na kocha wa Malaga, Manuel Pellegrini wanafikiriwa kuchukua jukumu hilo msimu ujao.
Klabu hiyo imesema kwamba hata wazuia mashabiki kuendelea na mgomo wao dhidi ya kocha huyo wa zamani wa Liverpool, hii imekuja baada ya wiki hii kuwaandikia barua Chama cha mashabiki wa Chelsea.
Ruksa: Mashabiki hawatazuiwa kuingia na mabango yao ya kumpinga Benitez kesho
Ofisa mmoja wa Chelsea alisema: “Napenda kuliweka hili bayana, klabu haina utaratibu wa kuzuia au kukutaza watu kuingia na mabango, kinachokatazwa ni mabaongo ya kutishia, matusi au ya kibaguzi au yatakayoziba wengine.
“Kwenye miaka ya nyuma mashabiki wamekuwa wakiruhusiwa kuingia na mabango ambayo waliyatumia kutoa dukuduku lao kuhusu klabu, na hatuna mpango wa kuzuia hilo.”
Chelsea hawataangalia suala la usalama kwenye mechi ya Jumamosi, licha ya maneno yaliyotolewa na Benitez, dhidi ya mashabiki.
Alhamisi alijaribu kumaliza bifu lake na mashabiki baada ya kukubali kufanya mahojiano na mwandishi wa BBC, Dan Walker. Alivunja sera ya klabu ya kuomba ruhusa kabla ya kufanya mahojiano na Chelsea hawakujua kama Benitez pale alipopanda gari baada ya mazoezi. Mahojiano hayo yatarushwa kwenye kipindi cha Football Focus, kesho.
Kwenye kipindi hiki Benitezi alisema: “Kila mtu anajua ni muhimu kamaliza kwenye timu nne za juu, au tatu, ilikuwa na uhakika wa kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Nataka kushinda kila mechi. Hivyo naweza kusema njia pekee ya kuibeba timu ni kuwaunga mkono wachezaji. Kama mashabiki wataendelea kuimba nyimbo za kuiponda timu – tulikuwa tnaongoza kwa mabao 2-0 lakini waliengelea kutuponda, sidhani kama watatushangilia tukiwa nyumbani.
“Uhusiano wangu na watu ndani ya klabu ni mzuri, uhusiano wangu na mmiliki ni mzuri na kila mara huwa naongea na Abramovich kuhusu soka, nafurahia sana. Sina tatizo na mtu.
Akifunguka: Benitez akizungumza na mwandishi wa BBC, Dan Walker, jana
Benitez alipewa jukumu la kuisaidia timu kumaliza kati ya timu nne za juu baada ya kuchukua mikoba ya Roberto Di Matteo, Novemba, mwaka jana.
Di Matteo alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kushinda michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopitia, lakini Benitez amesisitiza kwamba yeye anauzoefu unaombeba. Aliongeza: “Nilipokuja, tulikuwa tunakaribia kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, walitakiwa kufanya kitu na wakaamua kuwa mimi nina uzoefu nitafanya vizuri na nikaanza kazi yangu.
“Mwanzo ilikuwa ngumu kwa sababu kulikuwa na mechi moja kila baada ya siku tatu na baadaye ikawa rahisi kwa sababu wachezaji ni wazuri sana wanafanya mazoezi vizuri hata na hali ya hewa ndani ya klabu.”
Champion of Europe: Roberto Di Matteo retains huge support at Chelsea
‘It was difficult at the beginning because it was one game each three days, and after it was easier because you could see the players are really good, they train really well, they are keen to learn, so the atmosphere in the club is good.
When asked if he would be sacked, he replied: 'No. They know how we work and what we are trying to do.'
He added: 'The players are really happy in what we are trying to do. Sometimes you win, sometimes you cannot.
'There are no issues in the team. In terms of what we do, the players are fully behind the methods.
'If we stick together and support the players, we will be able to win games. Then at the end of the season I will leave and then they can criticise.'