Timu ya taifa ya Italia ilipigwa naradi wakati ikielekea Geneva, Uswiss kwa ajili ya mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidid ya Brazil, leo.
Wachezaji na viongozi wa timu hiyo walishangazwa na kilichotokea katika ndege yao hiyo kutoka Florence, Italia, lakini hakuna aliyedhurika.
Wahudumu wa kwenye ndege waliwatuliza wachezaji akiwemo Mario Balotelli, Andrea Pirlo na Stephan El Shaarawy – kwa kuwaeleza ilikuwa ni radi na hakukuwa na hatari.
Wametikiswa: Mario Balotelli na Cesar Prandelli wakiwa mazoezini baada ya radi
Sikuamiani: Prandelli aliwabishia wachezaji wake ambao walidai kuwa hawakuingiwa na hofu
Kocha wa Italia, Cesare Prandelli alisema: “Kwa kweli ilitia hofu na nilimbishia kila aliyedai kwamba hakuogopa. Iliwahi kunitokea hapo kabla lakini siyo kwa ukubwa huu.
Rubani Roberto Andolfato aliiambia Sky Sport: “Hali ilikuwa imedhibitiwa.”
Staili ya Samba: Andrea Pirlo (kulia) akiongoza mazoezi ya Italia inayojiandaa na kukutana na Brazil
Prandelli aliiambia figc.it: “Natakiwa kujiandaa vizuri kwa ajili ya mechi bila kuwapa faida yoyote Brazil.”
Gumzo kwa chat: Mshambuliaji wa Brazil, Neymar (kushoto) akipiga stori na Fred wakati wa mazoezi ya timu hiyo jana.
Mkono salama: Julio Cesar akiwa mazoezini