MSHAMBULIAJI Mario Balotelli ameendelea kucheka na nayvu baada ya jana kufunga mabao yote wakati Italia ikiilaza 2-0 Malta katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City aliifungia kwa mkwaju wa penalti nchi yake nyumbani katika dakika ya nane kabla ya kufunga la pili mapumziko.
Ushindi huo ambao ilishuhudiwa kipa Gianluigi Buffon akicheza mkwaju nwa penalti wa mshambuliaji wa Malta, Michael Mifsud, unaifanya Italia sasa iizidi Bulgaria pointi tatu kileleni mwa Kundi B.
Tabasamu tupu: Mario Balotelli akishangilia kufunga bao lake la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Malta, na chini akimtoka mtu
Wakati huo huo, Robin van Persie naye ameendelea kung'ara baada ya kuifungia Uholanzi mabao mawili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Romania hivyo kumpiku gwiji wa Uholanzi, Johan Cruyff kwa kuifungia mabao mengi nchi hiyo kihistoria.
Kiungo wa zamani wa Spurs, Rafael van der Vaart alifunga bao la kwanza dakika ya 11, wakati kipindi cha pili Van Persie alifunga mawili, la pili kwa penalti, na Jeremain Lens akapiga la nne katika dakika ya mwisho na kufanya Uholanzi iongoze kwa pointi saba kileleni mwa Kundi D.
Van Persie hakuwa mchezaji pekee wa Ligi Kuu England aliyeongozxa ushindi wa timu yake ya taifa, bali nyota wa Chelsea, Eden Hazard naye alifunga bao pekee katika ushindi wa Ubelgiji dhidi ya Macedeonia.
Shangwe: Robin van Persie akishangilia kumpiku Johan Cryuff kwa kuifungia mabao mengi Uholanzi na chini akishangilia na Arjen Robben
Winga huyo aliwatoka mabeki mawili kabla ya kufumua shuti kwa guu lake la kushotona kuiweka kileleni nchi yake katika Kundi A wakizipiku Wales na Croatia.
Beki wa kati wa Liverpool, Daniel Agger pia alifunga, akiiwezesha Denmark kupata pointi moja mbele ya Bulgaria kwa kufunga kwa penalti katika sare ya 1-1.
Mchezaji wa mkopo wa Watford, Matej Vydra alikuwa nyota mwingine wa England aliyefunga mabao mawili, katika ushindi wa 3-0 wa Jamhuri ya Czech dhidi ya Armenia wakati bao lingine lilifungwa na Daniel Kolar aliyetokea benchi.
Amefunga: Nyoa wa Chelsea, Eden Hazard ameifungia bao pekee Ubelgiji dhidi ya Macedonia
Katika kundi Ia England, Mabao ya Andriy Yarmolenko na Yevhen Khacheridi yaliwasaidia Ukraine waliokuwa 10 kushinda 2-1 dhidi ya Moldova, ambao bao lao la kufutia machozi lilifungwa na Alexandr Suvorov dakika za lala salama.
Robert Lewandowski alifunga penalti mbili siku ambayo Lukasz Piszczek pia alifunga wakati Lukasz Teodorczyk na Jakub Kosecki nao pia walifunga katika ushindi wa Poland dhidi ya San Marino wa 5-0.
Matawi ya juu: Mchezaji wa Watford, mshambuliaji wa Jamhuri ya Czech, Matej Vydra akishangilia baada ya kufunga bao lake la pili
Ujerumani imepaa kwa pointi tano dhidi ya Sweden kileleni mwa Kundi C, baada ya ushindi mnono wa mabao ya wakali wa Borussia Dortmund wa 4-1 dhidi ya Kazakhstan.
Marco Reus alifunga mawili na Mario Gotze na Ilkay Gundogan wakafunga mengine katika kikosi cha Joachim Low.
Vinara wa Kundi: Marco Reus wa Ujerumani akiifungia timu yake bao la nne dhidi ya Kazakhstan
Heinrich Schmidtgal aliifungia nchi yake bao la kufutia machozi. Ureno pia imeshinda, kwa mabao ya kipindi cha pili ya Bruno Alves na Hugo Almeida yaliyotengeneza ushindi wa 2-0 katika mchezo huo wa Kundi F dhidi ya Azerbaijan waliomaliza 10.