// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM SASA NDIO INAANZA MASHINDANO AFRIKA, NASIR ILIKUWA AMSHA MISULI TU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM SASA NDIO INAANZA MASHINDANO AFRIKA, NASIR ILIKUWA AMSHA MISULI TU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, March 05, 2013

    AZAM SASA NDIO INAANZA MASHINDANO AFRIKA, NASIR ILIKUWA AMSHA MISULI TU

    Mashabiki wa Azam; Wajiandae kushangilia katika mechi ngumu

    Na Mahmoud Zubeiry
    TANZANIA ina nafasi nne katika michuano ya klabu Afrika, mbili kwa ajili ya Zanzibar na mbili kwa Bara. Lakini baada ya mechi za Raundi ya kwanza, imebaki timu moja tu katika mashindano hayo, Azam FC ya Bara. 
    Nafasi ya kwanza imepotea kutokana na waliokuwa mabingwa wa Zanzibar, Super Falcon kujitoa kwa sababu za kukosa fedha za kuwawezesha kushiriki mashindano hayo.
    Kwa sababu hiyo, Jamhuri ya Pemba waliokuwa washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Zanzibar wakachukua nafasi ya Falcon katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Chama cha Soka Zanzibar kikatoa fursa kwa timu nyingine, yoyote kuanzia zilizoshika nafasi ya tatu kushiriki Kombe la Shirikisho, lakini hakuna Iliyojitokeza na nafasi hiyo ikapotea bure.
    Azam FC, sasa itamenyana na Barrack Young Controllers II ya Liberia katika Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, kufuatia jana kuitoa Al Nasir Juba ya Sudan Kusini.
    Azam jana imeitoa Al Nasir, kufuatia ushindi wa ugenini wa mabao 5-0, ambao unafanya ushindi wake wa jumla uwe 8-1, baada ya awali kushinda 3-1 Dar es Salaam. 
    Barrack Young Controllers II nayo imeifunga Johansens ya Sierra Leon bao 1-0 ugenini kufuatia sare ya bila kufungana katika mchezo wa awali ugenini.
    Kama ilivyotarajiwa na wengi, Azam ndio timu pekee iliyobaki kwenye michuano ya Afrika, baada ya jana kuitoa Al Nasir ya Juba.
    Katika mchezo huo, mabao ya Azam yalifungwa na Kipre Herman Tchetche, John Raphael Bocco kila mmoja mawili, moja kila kipindi na lingine Khamis Mcha ‘Vialli’.
    Jamhuri ya Pemba, ilikuwa timu ya kwanza ya Tanzania kuaga michuano ya Afrika, baada ya jana jioni kufungwa mabao 5-0 na wenyeji Kedus Giorgis nchini Ethiopia katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Matokeo hayo, yanamaanisha, Jamhuri imeaga kwa kufungwa jumla ya mabao 8-0, baada ya awali kutandikwa 3-0 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Gombani, Pemba.
    Wawakilishi wengine wa Bara katika michuano hiyo, Simba SC wametolewa pia baada ya kufungwa mabao 4-0 na Recreativo de Libolo ya Angola kwenye Uwanja wa Manispaa mjini Calulo, Angola.
    Matokeo hayo, yanaifanya Simba itolewe kwa jumla ya mabao 5-0, baada ya awali kufungwa bao 1-0 Dar es Salaam.
    Azam wataanzia ugenini mechi ya kwanza, kati ya Machi 15 na 17, mwaka huu kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye na wakivuka mtihani huo watakutana na mshindi kati ya FAR Rabat ya Morocco na Al Nasr ya Libya.
    Azam ilipata mteremko katika Raundi ya Kwanza kwa kukutana na timu dhaifu kutoka nchi mpya katika familia ya soka, ambayo ndio kwanza inajijenga.
    Lakini baada ya mteremko katika Raundi ya Kwanza, Azam sasa inakutana na timu ya ushindani, ambayo japo ni jina geni kwetu Watanzania, lakini inaonekana ni timu ya maana.
    Wazi, Azam inapaswa kujizatiti mno kuelekea hatua hiyo na kuziandaa akili za wachezaji wao katika mazingira ya kujua, wanakwenda kukutana na ugumu.
    Azam kama timu, inatia matumaini, kutokana na mambo mengi, kuanzia uwekezaji kwenye timu yenyewe, muundo wa timu na kadhalika.
    Hakuna shaka, wamiliki wa Azam wana kiu ya kufanya mambo makubwa katika soka ya Afrika. Wanataka kufanya vitu kama vile ambavyo vimewahi kufanywa na timu kama TP Mazembe ya DRC au Enyimba ya Nigeria.
    Ukitazama ule uwekezaji pale Chamazi, ambao hadi Mwanasoka Bora wa zamani Afrika, Abedi Pele aliusifia, unapata picha Azam wanataka nini.
    Lakini wao, wamiliki wa timu hawawezi kufanya kila kitu ndiyo maana wameajiri watu, kuna Menejimenti ya timu na wataalamu wengine, ambao sasa kila mmoja anatakiwa kufanya kazi yake vizuri.
    Ndiyo, kila mmoja afanya kazi yake vizuri ili Azam itimize ndoto za kufika mbali katika mashindano haya. Azam wanapaswa kujua mapema wanacheza na timu ya aina gani, inayocheza soka ya aina gani, ili maandalizi yao yawe ya kisayansi.
    Hawapaswi kukurupuka tu kuingia uwanjani kucheza, kisa wamekaa kambini na kufanya mazoezi mengi, bila ya kujua wanakwenda kucheza na timu ya aina gani na wacheze mfumo gani.
    Wachezaji wanatakiwa wajengwe kisaikolojia, wawe na kiu ya kucheza ili kushinda katika mashindano hayo makubwa. Hapa kuna kazi ya kufanya. Hapa ndipo mahala ambako tunaweza kuona tofauti ya Simba na Yanga zetu, dhidi ya timu kama Azam ambayo ni makini na yenye malengo.
    Kumekuwa na tatizo la majeruhi ndani ya Azam, wachezaji wanaumia sana. Hii lazima ijulikane chanzo ni nini? Mpangilio mbovu wa mazoezi, au udhaifu wa dawati la matabibu? 
    Unapoingia kwenye mashindano makubwa kama haya, lazima uwe na kikosi chako kamili cha kwanza na ikitokea dharula, basi akaosekane japo mchezaji mmoja tu.
    Tazama kwa sasa Azam, baada ya kuwakosa kwa muda mrefu John Bocco ‘Adebayor’, Waziri Salum na Abdulhalim Humud, tayari tena Brian Umony na Samih Hajji Nuhu majeruhi. Kweli, kuna kuumia kwa bahati mbaya, lakini pia kuna wachezaji kuumia kutokana na mapungufu ya watendaji katika timu. Lazima haya yatazamwe kwa kina, wakati huu ambao Azam imeingia Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho, kwani sasa ndiyo inaanza mashindano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM SASA NDIO INAANZA MASHINDANO AFRIKA, NASIR ILIKUWA AMSHA MISULI TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top