KIPA Petr Cech ajabu ni miongoni mwa majina sita katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa Arsenal, ili akaritihi mikoba ya Wojciech Szczesny msimu ujao.
Kipa huyo wa Chelsea amekuwa akifuatiliwa kwa makini na skauti wa Washika Bunduki hao wa London.
Cech anabaki kuwa kipa namba moja wa Chelsea na akihamia timu nyingine ya London utakuwa uhamisho ambao haukutarajiwa kabisa katika kumbukumbu za karibuni, lakini bado kuna mapendekezo kipa Thibault Courtois, ambaye yuko kwa mkopo Atletico Madrid kutoka Chelsea, anaweza kuziba pengo la Cech msimu ujao.
Vuguvugu la usajili: Arsenal inatumai kumsajili Petr Cech mwishoni mwa msimu
The Gunners wanajipa moyo wakimchukua Cech watamfungulia milango Courtois, mwenye umri wa miaka 20.
Chelsea inashawishika kwamba Courtois ni mtu aliyeandaliwa kwa muda mrefu kurithi mikoba ya Cech baada ya kufanya kazi nzuri misimu miwili kwa mkopo Hispania.
Mkataba wa Cech unaisha mwishoni mwa msimu wa 2016 na nafasi ya Chelsea kukubali kumuuza kipa huyo kwa moja wa wapinzani wao haitabiriki.
Hakubaliki: Wojciech Szczesny amekuwa akisugua benchi kwa mechi mbili zilizopita
Lakini ukweli kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekuwa macho mno katika usajili wa kujenga kikosi imara mwishoni mwa msimu.
Pepe Reina, Asmir Begovic, Victor Valdes, Rene Adler na Michel Vorm pia wamo katika orodha ya makipa wanaotakiwa.
Szczesny anakabiliwa na wakati mgumu kujinusuru Arsenal baada ya kufanya vibaya siku za karibuni. Mpoland huyo amekuwa akipigwa benchi mbele ya ndugu yake anayetoka naye nchi moja, Lukasz Fabianski katika kikosi cha Arsenal kwenye mechi mbili zilizopita dhidi ya Bayern Munich na Swansea.
Nyavu za The Gunners hazikuguswa katika mechi hizo jambo ambalo linaashiria Szczesny ataendelea kusugua benchi.
Chaguo la kwanza: Lukasz Fabianski amedaka mechi mbili mfululikzo bila kuruhusu hata bao moja Arsenal kufungwa
Katika mahojiano na gazeti la kila siku la Poland, Gazeta Wyborcza kuelekea ushindi wa Arsenal Uwanja wa Liberty, Szczesny alisema: ‘Nina furaha sana [hapa] kwenda sehemu yoyote pia. Naamini katika falsafa ya klabu na kwamba Arsenal itaanza kushinda tena. Nina deni la kulipa hapa kwa klabu. Sitaki kwenda sehemu yoyote pia. Hususan kama wananitaka mimi hapa, hakutakuwa na sehemu nyingine. Nina mkataba hadi Juni 2015.’