Walter Chilambo akipagawisha |
Shabiki wa kike akijiachia kwa Wababa |
Na Princess Asia
WASANII
wa Muziki wa Kizazi Kipya walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo Star
Search, Norman, Husna, Menina, Wababa, Geofrey na Walter jana walionyesha wao
ni moto wa kuotea mbali baada ya kuwapagawisha mashabiki zaidi ya elfu tatu
waliohudhuria katika ukumbi wa Club Maisha Dodoma.
Show
hiyo kali ilianza majira ya saa tano usiku, kwa mkali kutoka THT Ali Nipishe
anayetamba na kibao chake cha ‘MY’, na baadaye kumtambulisha Norman Severino
ambaye kwa mara ya kwanza alizindua wimbo wake wa ‘Si Wewe’.
Steji
ilizidi kuwaka moto pale kijana tokea Dodoma, Godfrey Levis alipopanda kuimba
wimbo wake wa ‘MAYA’ na kufuatiwa na malkia kutoka THT, Linah, aliyeimba nyimbo
zake zote kali.
Lakini
alikuwa ni mwanadada, Nsami aliyeonyesha kwamba wanawake waliopo kwenye tasnia
wajipange alipopanda kuimba wimbo wa ‘MUONGO’ na hatimaye mdada wa taarab, Husna
akawamaliza wanadodoma kwa kuimba wimbo wake wa ‘Nawamimina’, huku akisifiwa na
wengi kwa uwezo wake mkubwa wa kulimiliki jukwaa.
Kama
hiyo haitoshi, mashabiki pia waliburudishwa vya kutosha na mwimbaji bora wa
kiume wa mwaka, Barnaba, ambaye aliiimba nyimbo zake kama Magubegube na Sorry,
ambao unafanya vizuri sana sasa hivi na kuwafanya mashabiki kupiga kelele kwa
kumshangilia.
Ukumbi
ulizidi kulipuka kwa mayowe baada ya Barnaba kumtambulisha mwanadada mwingine,
Menina, ambaye wimbo wake wa Dream tonight unafanya vizuri kwenye vyomba vya
habari hapa nchini. Menina, ambaye alimsaidia Barnaba kuitikia wimbo wake wa
Wrong Number, alionyesha uwezo mkubwa katika kumiliki jukwaa.
Hadi
wakati mshindi wa tatu wa shindano la EBSS, Wababa Mtuka anapanda jukwaani
kuimba kibao chake cha ‘My Wife’ watu wa Dodoma walikuwa bado wakishangilia
namna alivoonyesha uwezo katika kuimba.
Wa
mwisho kabla ya mshindi wa milioni hamsini kupanda alikuwa ni Ben Paul, ambaye
aliwakonga nyoyo mashabiki wake kwa nyimbo zake kali kama Pete na Samboira
kabla ya kumkaribisha jukwaani Walter.
Mashabiki
hao waliokuwa wakimsubiri kwa hamu, walianza kupiga kelele Walter Walter, kabla
ya kuwatuliza kwa kuimba wimbo wake mpya wa ‘Siachi’ akifuatiwa wimbo wake
mwingine wa ‘Mamy Love’ ambao aliutoa kama zawadi kwa mashabiki zake wa Dodoma.
Walter
alipata wakati mgumu jukwaani ambapo mashabiki walimuomba azirudie nyimbo zake
zaidi ya mara tatu hali iliyoonyesha kukubalika kwa hali ya juu.
Mashabiki
wengi wakizungumza baada ya burudani hiyo walionyesha kuwakubali vilivyo
wasanii wa EBSS, huku wakiwatabiria makubwa.
‘Hakika
vijana wana vipaji na wanajua hasa kutoa burudani, wakipewa sapoti watafika
mbali sana’ alisema Maliki Abdul mkazi wa Dodoma aliyehudhuria burudani hiyo.
Ziara
hiyo ya washindi wa Epiq BSS inaelekea Dar mwisho wa mwezi huu kabla ya
kuelekea Mtwara.