Mfungaji wa mabao mawili ya Yanga juzi, Jerry Tegete kulia akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa Lyon. |
Na Prince Akbar
MECHI namba 119 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Februari 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka ushindi wa mabao 4-0 imeingiza sh. 68,438,000.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba, watazamaji 12,147 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 16,170,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,439,694.92.
Amesema kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo 10,982 walikata tiketi hizo na kuingiza sh. 54,910,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 8,222,162.26, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,933,297.36, Kamati ya Ligi sh. 4,933,297.36, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,466,648.68 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,918,504.53.