// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA NA AZAM KATIKA PICHA LEO TAIFA, LILIKUWA BONGE LA PATASHIKA HADI REFA KUTOKA KWA MSAADA WA POLISI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA NA AZAM KATIKA PICHA LEO TAIFA, LILIKUWA BONGE LA PATASHIKA HADI REFA KUTOKA KWA MSAADA WA POLISI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, February 23, 2013

    YANGA NA AZAM KATIKA PICHA LEO TAIFA, LILIKUWA BONGE LA PATASHIKA HADI REFA KUTOKA KWA MSAADA WA POLISI

    Kipa wa Yanga SC, Ally Mustafa 'Barthez' akiwa amedaka mpira mbele ya kiungo wa Azam FC, Humphrey Mieno na nyuma yake ni kiungo mwingine wa timu hiyo, Khamis Mcha 'Vialli', huku beki wake, Kevin Yondan (kushoto) akiwa tayari kutoa msaada katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ilishinda 1-0.

    Wachezaji wa Yanga, kutoka kulia Haruna Niyonzima, Oscar Joshua na Athumani Iddi 'Chuji' wakijadiliana wakati mchezo uliposimama kwa muda ili Barthez atibiwe baada ya kuumia

    Mshambuliaji hatari wa Azam FC, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast, akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Yanga, Kevin Yondan.

    Niyonzima (8) aliyeshikana mikono na Hamisi Kiiza akielekea eneo la mashabiki wa Yanga kushangilia baada ya kufunga

    Mabeki; David Mwantika wa Azam mbele akikabiliana na Kevin Yondan wa Yanga

    John Bocco akimiliki mpira mbele ya beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' 

    Mchezaji bora wa mechi ya leo; Haruna Niyonzima akiwa ameupitia mpira miguuni mwa mshambuliaji wa Azam, Seif Abdallah 

    Hamisi Kiiza kushoto akigombea mpira na David Mwantika, kulia ni Chuji na Salum Abubakar 'Sure Boy'

    Jerry Tegete akipiga shuti huku David Mwantika akiweka mguu

    Kipa Ally Mustafa 'Barthez' akiinuka baada ya kutibiwa na Daktari, Nassor Matuzya. Mbele yake ni Yondan akimfuatilia

    Simon Msuva akienda chini baada ya kupigwa kwanja na beki wa Azam

    Kikosi cha Azam leo 

    Kikosi cha Yanga leo

    Barthez amelala chini baada ya kuumia, huku mshambuliaji wa Azam, John Bocco 'Adebayor' akizungumza na refa Hashim Abdallah


    Niyonzima akimtoka Mieno

    Barthez anadondoka na mpira baada ya kuudakia juu

    Hamisi Kiiza akimueleza jambo beki wa Azam, Mwantika wakati kipa Mwadini Ally akiwa amelala chini baada ya kuumia. Wengine kushoto ni Didier Kvumbangu na refa Hashim Abdallah

    Barthez akiwapanga mabeki wake (hawapo pichani) wakati Azam wanapga mpira wa adhabu

    Kavumbangu akipasua ukuta wa Azam

    Kiiza kushoto akiwatoka mabeki wa Azam

    Chuji akinawa maji kupoza mishipa ya kichwa

    Kocha wa Azam, Stewart Hall akitoka uwanjani kinyonge baada ya mechi

    Refa Hashim Abdallah akisindikizwa na Polisi kutoka uwanjani baada ya mechi 

    Wachezaji wa Azam wakimzonga refa wakimtuhumu kumaliza mechi kabla ya muda

    Kocha wa Yanga, Ernie Brandts wa Uholanzi akiwapungia mikono mashabiki wake baada ya mechi

    Hamisi Kiiza kulia akigombea mpira na beki Joackins Atudo wa Azam

    Msuva akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Azam

    Joackins Atudo akimuondoa njianui Msuva 

    Jerry Tegete akimtoka Salum Waziri wa Azam

    Tegete amepiga tik tak mbele ya mabeki wa Azam

    Niyonzima akiambaa na mpira mbele ya wachezaji wa Azam

    Niyonzima anamtoka Mcha

    Niyonzima anamtoka Mcha

    Viungo bora; Salum Abubakar 'Sure Boy' wa Azam akigombea mpira na Frank Domayo wa Yanga. Nyuma ni Chuji akiwa tayari kuingilia

    Sure Boy anaambaa na mpira pembeni ya Tegete

    Frank Domayo akimvisha kanzu Kipre Tchetche

    Sure Boy anamtoka Kavumbangu

    Sure Boy anawatoka viungo wa Yanga Domayo na Chuji kulia. Mbele ni Yondan

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA NA AZAM KATIKA PICHA LEO TAIFA, LILIKUWA BONGE LA PATASHIKA HADI REFA KUTOKA KWA MSAADA WA POLISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top