Rais wa TFF anayemaliza muda wake, Leodegar Tenga |
Na Boniface Wambura
UCHAGUZI wa
viongozi wa Chama cha Waamuzi wa Soka Tanzania (FRAT) unafanyika Februari 14
mwaka huu mjini Morogoro kama ulivyopangwa, tofauti na taarifa wanazopewa
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho.
Kwa mujibu wa
Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya FRAT, Damas Ndumbaro, wajumbe wa Mkutano Mkuu
wa FRAT wanatakiwa kufika Morogoro keshokutwa (Februari 12 mwaka huu) . Pia
wapiga kura na wagombea wanatakiwa kulipia ada za uanachama kwa mwaka 2013
kabla ya uchaguzi.
Wagombea ni Army
Sentimea na Said Nassoro (uenyekiti) wakati wanaoomba nafasi ya Makamu
Mwenyekiti ni Juma Chaponda, Juma Mpuya na Tifika Kambimtoni.
Abdallah Mitole,
Charles Ndagala na Hamis Kisiwa wanawania ukatibu mkuu, nafasi ya Mhazini
inagombewa na Jovin Ndimbo. Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) ni Kamwaga Tambwe wakati nafasi ya uwakilishi wanawake
yupo Isabela Kapera.
Wagombea wa nafasi
ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Emmanuel Chaula na Samson Mkotya.