Ngowi |
Na Prince Akbar
KAMISHENI
ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), imewataka mabingwa wake wote wawe
wametetea mikanda yao ya ubingwa ifikapo tarehe 30 Marchi kwaka huu ili kuepuka
kunyanganywa.
Rais
wa TPBC, Onesmo Ngowi amesema kwa kipindi kirefu mabingwa kadhaa wamekuwa
wanakaa na mikanda bila kuitetea, hivyo wanataka ieleweke kuwa muda wa kukaa na
ubingwa wa TPBC ni miezi sita, tu na sio mwaka mmoja.
Amesema
bingwa wa kweli anatakiwa awe anafuata sheria, kanuni na taraibu za ubingwa alionao
na sio kujiita bingwa wakati hufuati masharti yaliyowekwa.
Amesema
katika kipindi hiki cha mwaka 2013 tunawataka mabondia waheshimu sheria za
mikataba wanayotiliana sahihi na mapromota. “Tunataka ngumi ziboreshwe kakini
pamoja na changamoto nyingi zilizoko, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wadhamini,
mabondia wakiheshimu mikataba yao mchezo wa ngumi utakua na kuwavutia wadhamini,”amesema.
Ngowi
ameongeza wanapenda pia kuwaomba wenye mapenzi mema na nchi hii wajitolekeze
kwa wingi ili kushirikiana nao, ili kuiweka Tanzania kwenye chati ya dunia kama
zilivyo nchi nyingine.