// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STARS NA CAMEROON ZAINGIZA HASARA TUPU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STARS NA CAMEROON ZAINGIZA HASARA TUPU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 07, 2013

    STARS NA CAMEROON ZAINGIZA HASARA TUPU

    Beki wa Cameroon, Assou Ekotto akimiliki mpira mbele ya Mrisho Ngassa wa Tanzania

    Na Mwandishi Wetu
    MECHI ya kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania, Taifa Stars na Cameroon, Simba Wasiofungika  iliyochezwa jana Uwanja wa Taofa, Dar es Salaam na wenyeji kushinda bao 1-0, imeingiza Sh. 148,144,000, ambayo dhahiri ni hasara.
    Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zaidi ya Sh, Milioni 250 zilitumika kama gharama za kuandaa mchezo huo. 
    Taarifa ya TFF, imesema fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 23,092 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
    Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 22,598,237.29, maandalizi ya mchezo sh. 58,000,000 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,340,900.
    Nyingine ni bonasi kwa wachezaji wa Taifa Stars sh. 18,831,864.41, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 8,274,659.66, asilimia 15 ya uwanja sh. 6,205,994.75 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 2,068,664.92.
    Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,823,978.98 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,241,199 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
    Mapato hayo madogo, dhahiri yametokana na kutokuja kwa wachezaji wawili nyota na maarufu zaidi wa Cameroon, Samuel Eto'o wa Anzhi ya Urusi na Alex Song wa Barcelona. 
    Mashabiki wengi walilipuuza pambano hilo, baada ya kuvuja mapema kwa taarifa za kutokuja kwa wawili hao, ambao wanapendwa mno nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: STARS NA CAMEROON ZAINGIZA HASARA TUPU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top