Eto'o |
Na Boniface Wambura
WAKATI
kundi la kwanza la timu ya Cameroon lenye watu 13 linaingia nchini leo
(Februari 3 mwaka huu) saa 4.40 usiku, kundi la pili linaloongozwa na nahodha
wa timu hiyo Samuel Eto’o linatua kesho (Februari 4 mwaka huu) saa 3.45 asubuhi
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Eto’o
anayechezea timu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi atatua kwa ndege ya Kenya
Airways akiwa na Herve Tchami wa Budapest Honved ya Hungary, beki Nicolas
Nkoulou wa Marseille ya Ufaransa, mshambualiji Jean Paul Yontcha wa SC
Olhanense ya Ureno na daktari wa timu Dk. Boubakary Sidik.
Saa
moja baadaye baada ya Eto’oo kutua na wenzake, Kocha wa timu hiyo Jean Paul
Akono na msaidizi wake Martin Ndtoungou watawasili saa 4.40 asubuhi kwa ndege
ya Kenya Airways wakitokea Afrika Kusini.
Kesho
pia kuna kundi lingine litakaloingia saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM ambalo
lina beki Jean Kana Biyick wa Rennes ya Ufaransa, mshambuliaji Fabrice Olinga
wa Malaga FC ya Hispania, beki Allan Nyom wa Udinese ya Italia ambaye yuko kwa
mkopo Granada ya Hispania na beki wa kushoto Henri Bedimo wa Montpellier ya
Ufaransa.
Wachezaji
waliobaki wakiongozwa na kiungo wa Barcelona, Alexandre Song watawasili
Februari 5 mwaka huu kwa muda tofauti kwa ndege za KLM na Kenya Airways.
Wakati
huo huo: Waamuzi kutoka Rwanda wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) ndiyo watakaochezesha pambano katika Tanzania na Cameroon
litakalochezwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi
wa katikati atakuwa Munyemana Hudu wakati wasaidizi wake ni Simba Honore na
Ndagizimana Theogine wakati mwamuzi wa mezani ambaye pia anatambuliwa na FIFA
atakuwa Oden Mbaga wa Tanzania.
Hudu
na wenzake watawasili nchini kesho (Februari 4 mwaka huu) saa 12.40 jioni kwa
ndege ya RwandAir na wamepangiwa kufikia kwenye hoteli ya JB Belmont. Mechi
ambayo ni moja kati ya nyingi zitakazochezwa siku hiyo (FIFA Date) itafanyika
kuanzia saa 11 kamili jioni.