Samatta na Ulimwengu kulia |
Na Boniface Wambura
WASHAMBULIAJI
wa Taifa Stars, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanatarajia kutua nchini
kesho (Februari 3 mwaka huu) tayari kwa mechi ya Cameroon itakayochezwa
Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Samata
na Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
(DRC) watawasili saa 11.10 jioni kwa ndege ya PrecisionAir na kwenda moja kwa
moja kambi hoteli ya Tansoma.
Wachezaji
wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanaanza kuripoti
kambini leo jioni (Februari 2 mwaka huu) mara baada ya mechi kati ya Yanga na
Mtibwa Sugar.
Mechi
hiyo iliyo katika Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
pia itatumika kwa ajili ya kutoa ujumbe wa vita dhidi ya Malaria viwanjani,
ugonjwa unaoongoza barani Afrika kwa kusababisha vifo vya watoto na wajawazito.
TFF
kama ilivyo Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA), Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na FIFA imekuwa msitari wa
mbele katika kueneza kampeni ya vita dhidi ya Malaria inayoongozwa United
Against Malaria (UAM). Rais wa TFF, Leodegar Tenga na nahodha wa Cameroon,
Samuel Eto’o ni miongoni mwa mabalozi wa vita dhidi ya Malaria barani Afrika.
Wakati
huo huo: Kundi la kwanza la Cameroon likiongozwa na kiungo wa zamani wa
Toulouse ya Ufaransa ambaye sasa yuko Al Ahli ya Falme za Kiarabu (UAE),
Achille Emana na Meneja wa timu hiyo Rigobert Song litatua nchini kesho
(Februari 3 mwaka huu) saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM.
Wachezaji
wengine katika kundi hilo ni Vincent Aboubakary anayechezea timu ya
Valenciennes iliyoko Ligi Kuu ya Ufaransa, kipa Charles Itandje anayedakia timu
ya POAK FC ya Ugiriki, Kocha wa viungo Sylvain Monkam.
Mshambuliaji
wa Anzhi Makhachkala ya Urusi ambaye ndiye nahodha wa Cameroon, Samuel Eto’o
ataongoza kundi la pili litakalowasili nchini Februari 4 mwaka huu (saa 3.45
asubuhi) kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi, Kenya.
Wengine
katika ndege hiyo Herve Tchami wa Budapest Honved ya Hungary, beki Nicolas
Nkoulou wa Marseille ya Ufaransa, mshambualiji Jean Paul Yontcha wa SC
Olhanense ya Ureno na daktari wa timu Dk. Boubakary Sidik wakati Kocha wa timu
hiyo Jean Paul Akono na msaidizi wake Martin Ndtoungou watawasili saa 4.40 asubuhi
kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Afrika Kusini.
Februari
4 mwaka huu kuna kundi lingine litakaloingia saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM
ambalo lina beki Jean Kana Biyick wa Rennes ya Ufaransa, mshambuliaji Fabrice
Olinga wa Malaga FC ya Hispania, beki Allan Nyom wa Udinese ya Italia ambaye
yuko kwa mkopo Granada ya Hispania na beki wa kushoto Henri Bedimo wa
Montpellier ya Ufaransa.
Wachezaji
waliobaki wakiongozwa na kiungo wa Barcelona, Alexandre Song watawasili
Februari 5 mwaka huu kwa muda tofauti kwa ndege za KLM na Kenya Airways.