UEFA imeitupilia mbali rufaa ya Schalke dhidi ya Didier Drogba kuichezea timu yake mpya, Galatasaray katika mechi ya sare ya 1-1 ya Ligi ya Mabingwa, baina ya timu hizo mapema mwezi huu.
Timu hiyo ya Ujerumani iliamini timu hiyo ya Uturuki inaweza kupoteza mchezo huo, kwa madai Drogba alisaini kwao siku 12 baada ya dirisha la usajili kufungwa.
Klabu hiyo ya Ujerumani, ilidai Galatasary haikutangaza ujio wa Drogba katika tovuti yao hadi Februari 12, ingawa sheria za UEFA zinasema mwisho wa usajili Februari 1 kwa ajili ya hatua ya mtoano.
Didier Drogba akimiliki mpira katika sare ya 1-1 kati ya Galatasaray na Schalke miini Istanbul.
Drogba akikanyaga ardhi ya Uwanja wa Ndege wa Ataturk Jijini Istanbul kusaini Galatasaray mapema mwezi huu