Wayne Rooney ametambulishwa kama mtuwa Manchester United wa kuogopwa zaidi kuelekea mchezo wa leo
Marca
INAONEKANA kama Real Madrid, wanamuhofia Wayne Rooney kuelekea kwenye pambano lao la kesho lwa Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku moja ya magazeti ya Jiji la Madrid wakimtaja kama Zimwi au Pepo lililojengwa kama Kontena na kujazwa unga wa risasi, ambalo linaelekea kuilipua Bernabeu.
Na kuchochea moto wa pambano la mzunguko wa kwanza wa hatua ya 16 bora, gazeti la Marca limemuweka mshambuliaji huyo wa Manchester United kwenye ukurasa wake wa mbele katika gazeti hilo huku kukiwa na kicha cha habari kisemacho ‘The Bad Boy' anakuja na washikaji zake 5,000.
Gazeti hilo limemtaja mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England kama Mchezaji na Mhuni kwa wakati mmoja, Marca wameandika kwamba hakuna tofauti kati ya Rooney na mashabiki 5000 wa Man United wanaotegemewa kuwapo uwanjani kesho usiku.
Lakini pia wametoa onyo kwamba mshambuliaji huyo aliye kwenye fomu atakutana na wachezaji kadjhaa wa Reali Madrid ambao watampa wakati mgumu sana.
Kati ya hao ni beki Pepe, ambaye Rooney aliwahi kumuita chizi kwenye akaunti yake ya Tweeter, Januari mwaka jana baada ya ya Mreno huyo kumkanyaga makusudi Lionel Messi wakati wa robo fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Barcelona.
“Pepe. Chizi kweli. Kunawakati watu wanakuzidi,” ilisomeka Tweet ya Rooney ambayo leo imewekwqa kwenye ukurasa wa pili wa gazeti la Marca.
Mwaka 2006, Rooney alipewa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko Pepe, ambaye wakati huo alikuwa akichezea Porto. Hii ilikuwa baada ya wawili hao kulika pamoja angani wakati wa mechi ya maandalizi ya msimu mpya katika michuano ya Amsterdam.
Wiki moja kabla ya tukio hilo Rooney alihusika kwenye tukio lingine dhidi ya Ricardo Carvalho – ambaye anaweza kuwepo kwenye kikosi cha Real Madrid cha kesho, hii ilikuwa baada ya Rooney kumpanda beki huyo wakati wa Robo fainali ya Kombe la Dunia 2006, dhidi ya Ureno na huku Ronaldo akimsisitiza mwamuzi kumpa Rooney kadi nyekundu.
Gazeti hilo linalopatikana katika Jiji la Madrid leo limetoa idadi kubwa ya kurasa zake kuelezea jinsi gani wanaamini kwamba Rooney atakuwa hatari kwenye mechi ya Jumatano usiku, wakati Man United wakatakapokutana uso kwa uso na Real Madrid kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya pale Bernabeu.
Rooney mwenyewe anaweza asijali sana, hasa kutokana na kuwa kwenye kiwango chake bora cha kufanya vizuri kwenye mechi kubwa.
Katimba: Rooney alipewa kadi nyekundu kutokana na tukio hili na beki wa Ureno Ricardo Carvalho wakati wa Kombe la Dunia mwaka 2006.
Real Madrid wamefanya mazoezi kwenye jua kali katika uwanja wa mazoezi leo asubuhi, huku kikosi chote cha Jose Mourinho kikiwepo uwanjani wakati wa dakika 15 ya kupasha misuli moto ambayo vyombo vya habari waliruhusiwa kushuhudia.
Watu wengi watakuwa wakimtazama Cristiano Ronaldo, katika masaa 24 yajayo na mchezaji huyo wa Man United alionekana kuwa katika hali ya kawaida leo asubuhi kuelekea kwenye mechi ambayo itamgusa sana kwenye maisha yake yote ya soka.
Man United, kwa upande wao walitarajiwa kufanya mazoezi Manchester leo asubuhi kabla ya kukwea pia na kuenda Hispania mchana wa leo.
Sir Alex Ferguson ataongea na waandishi wa habari juu ya mechi hiyo baadaye
Rooney amefunga mabao 14 katika mechi 27 za hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya – akiwa na wastani wa asilimia 52, kitu kinachomfanya kuwa mbele ya wapinzani wake.
Kwa kumilinganisha na wengine, Lionel Messi anawastani wa asilimia 46, Cristiano Ronaldo asilimia 45.
Didier Drogba ana asilimia 33 ya kufunga mabao baada ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, wakati Robin van Persie ana asilimia 24.
Mabao ya Rooney kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
2010-2011
Aprili 6-Chelsea (A) Robo fainali, Ushindi wa 1-0 (bao moja)
Aprili 26 - Schalke (A) Nusu fainali, ushindi wa 2-0 (bao moja)
Mei 28- Barcelona (Wembley) fainali, kufungwa 3-1 (bao moja)
2009-2010
Februari 16-AC Milan (A) 16 Bora, ushindi wa 3-2 (mabao mawili)
Machi 10 - AC Milan (H) 16 Bora, ushindi wa 4-0 (mabao mawili)
Machi 30 - Bayern Munich (A) Robo fainali, kufungwa 1-2 (bao moja)
2008-2009
Aprili 7 - FC Porto (H) Robo fainali, sare 2-2 (bao moja)
2007-2008
Aprili 1 - Roma (A) Robo fainali, Ushindi wa 2-0 (bao moja)
2006-2007
Aprili 4 - Roma (A) Robo fainali, kufungwa 2-1 (bao moja)
Aprili 10 - Roma (H) Robo fainali, ushindi wa 7-1 (bao moja)
Aprili 24 - AC Milan (H) nusu fainali, ushindi wa 3-2 (mabao mawili)
Ukurasa wa mbele wa gazeti la kila siku la Marca la mjini Madrid lilivyomzungumzia Rooney
VIDEO: Rooney akimtoa nje Pepe mjini Amsterdam mashindano ya mwaka 2006
Pepe akiwa amelala chini baada ya kuumizwa na Rooney katika mashindano ya Amsterdam kati ya Manchester United na Porto mwaka 2006
Rooney alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa tukio hilo dhidi ya beki wa Ureno, Ricardo Carvalho katika Kombe la Dunia mwaka 2006
Cristiano Ronaldo akimiliki mpira kwenye mazoezi ya Real jana asubuhi