// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RIGOBRT SONG YUKO TAYARI KUSAINI SIMBA, AU YANGA HATA AZAM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RIGOBRT SONG YUKO TAYARI KUSAINI SIMBA, AU YANGA HATA AZAM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, February 05, 2013

    RIGOBRT SONG YUKO TAYARI KUSAINI SIMBA, AU YANGA HATA AZAM

    Song leo; Nipo tayari kucheza klabu yoyote Tanzania

    Na Mahmoud Zubeiry
    BEKI wa zamani wa Liverpool ya England, Rigobert Song Bahanag amesema yuko tayari kusaini klabu yoyote ya Tanzania, iwe Yanga, Azam hata Simba SC achezee kumalizia soka yake, iwapo watampa ofa ya kuridhisha.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo mchana mjini Dar es Salaam, Song ambaye kwa sasa amestaafu soka na kuwa Meneja wa timu ya taifa ya Cameroon, amesema kama ipo klabu kweli ya hapa itakayoonyesha nia naye, atakuwa tayari kwa mazungumzo. 
    "Kwa nini nikatae ofa ya kunirudisha uwanjani?" alihoji Song baada ya kuulizwa iwapo itatokea klabu ya Tanzania kumuhitaji amalizie soka yake. "Sijui timu za hapa, ila yoyote ikinitaka inifuate hotelini tuzungumze,"aliasema.
    Song alisema ameamua kustaafu ingawa anajiona bado yuko fiti ili kuwapisha wachezaji wengine, kwani anaona umri wa miaka 36 ni mkubwa na amecheza kwa muda mrefu. 
    Song, aliyezaliwa Julai 1, mwaka 1976, baada ya kustaafu soka kwa sasa mbali na kuwa Meneja wa timu ya taifa ya nchi yake aliyoichezea kuanzia mwaka 1993 hadi 2010, pia ni mchambuzi wa masuala ya kabumbu katika Televisheni ya Channel Orange Sports.
    Kisoka, Song aliibukia katika klabu ya Metz ya Ufaransa mwaka 1994, ambako alidumu hadi 1998 alipohamia Salernitana aliyoichezea hadi 1999 alipotua Liverpool, ambako hata hivyo hakudumu mwaka 2000 akahamia West Ham United ya nchini humo pia, aliyoichezea hadi 2001 akahamia FC Koln kwa mkopo, baadaye Lens ya Ufaransa mwaka 2002 hadi 2004, Galatasaray ya Uturuki 2004 hadi 2008 na kumalizia soka yake Trabzonspor ya Uturuki pia, 2008 hadi 2010.
    Jumla katika ngazi ya klabu, Song amecheza mechi 417 na kufunga mabao 11, wakati timu ya taifa amecheza mechi 138 na kufunga mabao matano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: RIGOBRT SONG YUKO TAYARI KUSAINI SIMBA, AU YANGA HATA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top