Kikosi cha Yanga SC |
Na Prince Akbar
KLABU
za Yanga na Mtibwa Sugar zinapambana kesho (Februari 2 mwaka huu) katika moja
ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mwamuzi
Ronald Swai kutoka Arusha ndiye atakayechezesha mechi hiyo inayotarajiwa kuwa
na upinzani mkali, kwani wakati Yanga ikiongoza ligi hiyo, wapinzani wao Mtibwa
Sugar katika mechi iliyopita walilala mbele ya Polisi Morogoro ambayo ni ya
mwisho katika msimamo wa ligi kwa sasa.
Polisi
Morogoro itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini
Morogoro wakati Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi
kati ya Mgambo Shooting na Ruvu Shooting inayofundishwa na Charles Boniface
Mkwasa.
Keshokutwa
(Jumapili) kutakuwa na mechi mbili. Simba itaumana na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam huku Tanzania Prisons ikiikabili Coastal Union katika
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Wakati
huo huo; Villa Squad na Moro United zinaumana kesho (Februari 2 mwaka huu)
Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika moja ya mechi za kundi B za Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) inayoanza mzunguko wa lala salama.
Kundi
A litakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Burkina Faso itakayochezwa Uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya, Majimaji na Kurugenzi katika Uwanja wa Majimaji mjini
Songea, na Polisi Iringa dhidi ya Mkamba Rangers kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Samora mjini Iringa.
Mechi
nyingine ya Kundi B itakuwa Transit Camp na Ndanda itakayochezwa Uwanja wa
Mabatini mkoani Pwani. Kundi C ni Polisi Dodoma na Kanembwa JKT (Uwanja wa
Jamhuri, Dodoma), Morani dhidi ya Mwadui (Uwanja wa Kiteto, Manyara), Polisi
Mara na Pamba (Uwanja wa Karume, Musoma), Polisi Tabora na Rhino Rangers
(Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).
Ligi
hiyo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa Machi mwaka huu ambapo mshindi wa kila
kundi atapanda daraja kucheza Ligi Kuu msimu ujao.