KUFUNGWA kwa Barcelona na AC Milan ndiyo matokeo ya kushangaza zaidi kwenye mechi za hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mabao yaliofungwa na wachezaji wa zamani wa Portsmouth – Kevin Prince Boateng na Sulley Muntari – yameifanya miamba ya Catalan ikiwa na mlima mkubwa wa kupanda baada ya wiki tatu.
Lakini, hii haina maana kuwa Barca ndio wamshaaga mashindano. Kuna mifano kadhaa kwenye historia ambayo inawapa matumaini mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2009 na 2011 matumaini. Mija ya mifano ya kukumbukwa zaidi ni kutoka kwenye michuano ya Kombe la UEFA mwaka 1996, pale Zinedine Zidane alipoisaidia Bordeaux kuitupa AC Milan nje ya michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 nchini Ufaransa hii ikiwa ni baada ya kufungwa mabao 2-0 Italia kwenye mechi ya kwanza.
Futa machozi mwenzangu: Lionel Messi akipewa pole na beki wa AC Milan Philippe Mexes, San Siro jana
Muunganiko wa Portsmouth: Wafungaji wa mabao ya AC Milan, Kevin-Prince Boateng (kushoto) na Sulley Muntari wakishangilia
Bao la Didier Tholot katika kipindi cha kwanza, na mengine mawili kutoka kwa Christophe Dugarry katika kipindi cha pili, yalitosha kufuta mabao ya Stefano Eranio na Roberto Baggio yaliyofungwa kwenye mechi ya kwanza.
Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza timu kutoka Italia ilishindwa kusonga mbele kwenye michuano ya Ulaya baada ya kushinda mabao 2-0 nyumbani.
Hatahivyo, kwenye miaka ya karibuni AC Milan ikiwa chini ya Carlo Ancelotti, ilishindwa kulinda ushindi wake wa mabao 4-1 iliyoupata nyumbani dhidi ya Deportivo La Coruna wakati war obo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2004.
Na historia ya Barcelona inaweza kuwapa moyo Messi na jeshi lake pia.
Hamasa ya Barca: Zinedine Zidane (kati kati) alifanya uchawi wake kuibeba Bordeaux dhidi ya Milanm, mwaka 1996
Kinachotoa moyo
Barcelona wameshinda mechi zao tatu tu kati ya 14, kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, waliwahi kutoka sare na kufungwa Emirates mwaka 2010 na 2011.
Ni mara nane tu kwenye historia ya Ligi ya Mabingwa, ambapo timu ilisonga mbele licha ya kufungwa mechi ya kwanza kwa mabao mawili au zaidi kwenye mechi ya kwanza. Barcelona, ndio timu pekee kufanya hivyo mara mbili.
Walitoka nyuma kwa mabao 3-1 dhidi ya Dynamo Kiev mwaka 1993 na kushinda kwa mabao 4-1, Nou Camp.
Kocha wa sasa wa Swansea, Michael Laudrup alifunga bao la kwanza kabla ya mabao kutoka kwa Ronald Koeman na Jose Mari Bakero alifunga mawili, Sergey Rebrov alifunga bao moja la Dynamo lakini Barca walisonga mbele.
Kurejea wafalme: Rivaldo na Luis Figo waliongoza mashambulizi wakati Barca wakiitandika Chelsea mabao 5-1, Nou Camp mwaka 2000
Barca waliwahi kutoka nyuma na kushinda kwa mabao 5-1, hii ilikuwa baada ya kufungwa mabao 3-1 kwenye robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2000.
Bao la faulo iliyopigwa na Gianfranco Zola na mengine mawili kutoka kwa Tore Andre Flo yalionyesha kama Chelsea wangesonga mbele katika hatua inayofuata, lakini kikosi cha Barca kikiwa na Luis Figo na Rivaldo, ambao wote walifunga kwenye pambano la Nou Camp, yalitosha kuivusha Barca.
Ni timu mbili tu za England ambazo zilishinda mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufungwa mabao mawili au zaidi kwenye mechi ya kwanza.
Kila kitu ni historia… John Terry na Frank Lampard wakishangilia ushindi dhidi ya Napoli
Mkali wa vichwa: Didier Drogba akifunga na kushangilia wakati wa ushindi wa mabao 4-1 Stamford Bridge msimu uliopita.
Maumivu Hispania
Barca wako kwenye hatari kubwa ya kutolewa kwenye ligi ya mabingwa na maadui zao Real Madrid nao wanakibarua kigumu baada ya kutoka sare ya mbao 1-1 dhidi ya Manchester United, kwenye mechi ya kwanza.
Mara ya mwisho Real Madrid na Barcelona wameshindwa kuvuka hatua hii ilikuwa mwaka 2007, wakati ambao AC Milan walitwaa ubingwa huo baada ya kuifunga Liverpool kwenye fainali.
Leeds United walishinda 4-1 dhidi ya mwaka 1992 baada ya kufungwa mabao 3-0 kwenye mechi ya kwanza na Chelsea walishinda 4-1 nyumbani baada ya kufungwa 3-1 na Napoli ugenini msimu uliopita.
Arsenal pia wanatakiwa kugeuza matokeo yao baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 nyumbani, kutoka kwa Bayern Munich.
The Gunners wanahasara moja kubwa ambayo ni kucheza mechi yao ya marudiano ugenini na haijawahi kutokea kwenye ligi ya mabingwa klabu kugeuza matokeo ya namna hii.
Lakini kuna matumaini kwa Celtic. Pia na kichapo cha Milan kutoka kwa Depor, mafanikio ya Leeds dhidi ya Stuttgart, mwaka 1992 yanatarajiwa.
Kila la kheri: Arsenal na Celtic wanakibarua kigumu dhidi ya Bayern na Juve