// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PATASHIKA MALI NA NIGERIA AFCON LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PATASHIKA MALI NA NIGERIA AFCON LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, February 06, 2013

    PATASHIKA MALI NA NIGERIA AFCON LEO


    Football | Afcon

    Durban ready for battle of the birds


    NUSU Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Nigeria, Tai Mkubwa na Tai wa Mali inapigwa kwenye Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban leo.
    Vijana wa Patrice Carteron wanaingia kwenye mchezo wa leo baada ya kuwatoa wenyeji, Afrika Kusini kwenye Robo Fainali kwa mikwaju ya penalti, wakati vijana wa Stephen Keshi waliwaduwaza Ivory Coast waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kufika mbali.
    Nigeria ndio inapewa nafasi kubwa sasa kutoka mechi hii inayozikutanisha timu zote za Magharibi mwa Afrika kutinga fainali.
    Timu hizo zote zilimaliza katika nafasi ya pili kwenye hatua ya makundu.
    Mshambuliaji wa Nigeria, Emmanuel Emenike, anaongoza kwa mabao katika mashindano haya akiwa amefunga matatu hadi sasa na anapewa nafasi kubwa ya kuendelea kufunga hadi leo.
    Keshi atakuwa na kikosi chake kamili baada ya kurejea kwa Fegor Ogude aliyekosa Robo Fainali kwa kutumikia adhabu ya kadi, lakini anaweza kupanga kikosi kile kile kilichoitoa Ivory Coast.
    Lakini Mohamed Sissoko wa Mali na Samba Diakite wako shakani katika mchezo wa leo na wanakabiliwa na changamoto ya kupambana na majeruhi dakika za mwishoni ili wacheze mechi ya leo.
    Nahodha wa Mali, Seydou Keita, ambaye amefunga mabao mawili katika Afcon hii, hakubaliani na kwamba kila mmoja anaipa nafasi Nigeria.
    "Watu wanaendelea kusema Nigeria watatufunga Jumatano, kwa sababu kocha wao, Stephen Keshi anaifahamu nje ndani timu ya Mali aliyoifundisha awali, lakini hilo si kweli," alisema Keita.
    Keshi pia anabebwa na rekodi, kwani Nigeria haijawahi kufungwa na Mali kwenye mashindano haya tangu mwaka 2002.
    Nigeria imeifunga Mali mara mbili katika mara nne walizokutana kwenye Afcon tangu 2002, mechi nyingine zikiisha kwa sare ikiwemo ya 0-0 huko Sekondi-Takoradi, Ghana mwaka 2008 timu hizo zilipotana mara ya mwisho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: PATASHIKA MALI NA NIGERIA AFCON LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top