FAINALI ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu itazikutanisha Burkina Faso na Nigeria. Hiyo inafuatia Burkina Faso kuing'oa Ghana kwa mikwaju ya penalti 3-2 jana usiku kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.
Walipata ushindi huo, baada ya Emmanuel Agyemang Badu kukosa penalti ya tatu kwa kupiga shuti dhaifu.
Lakini Burkinabe watamkosa Jonathan Pitroipa kwenye Fainali Jumapili baada ya kupewa kadi nyekundu dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.
Wachezaji wa Burkina Faso wakishangilia ujshindi wa matuta uliowapeleka fainali
Ghana ilipata bao la kuongoza dakika ya 13 lililofungwa na Mubarak Wakaso kwa penalti, ambayo ni ya tatu katika mashindano haya, kufuatia beki wa Burkina Faso, Paul Koulibaly kumchezea rafu Christian Atsu.
Burkina Faso ilisawazisha dakika ya 60, wakati Aristides Bance alipofunga kwa shuti la kawaida tu akiwa kwenye eneo la penalti.
Zoezi la mikwaju ya penalti lilianza vibaya kwa Ghana, baada ya Isaac Vorsah kupaisha mkwaju wake na Burkina Faso wakafunga kupitia kwa Bakary Kone, Henri Traore na Bance.
Mcheza wa Burkina Faso, Aristide Bance (kulia) akifunga penalti ya ushindi
Mubarak Wakaso wa Ghana, akifunga bao la kwanza kutoka umbali wa mita 12
Una uhakika refa? Kiungo wa Burkina Faso, Jonathan Pitroipa akilalamika baada ya kupewa kadi ya pili ya njano kwa kujirusha
Huzuni: Wachezaji wa Ghana wakisikitika baada ya kupoteza penalti zao
Kabla ya janga...Mashabiki wa Ghana wakishangilia
Baada ya janga...Shabiki la Ghana katika sura ya huzuni