// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MWENYE TIMU AMUITA BALOTELLI NYANI AC MILAN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MWENYE TIMU AMUITA BALOTELLI NYANI AC MILAN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, February 06, 2013

    MWENYE TIMU AMUITA BALOTELLI NYANI AC MILAN


    Shocking: Paolo Berlusconi
    Shocking: Paolo Berlusconi

    MSHAMBULIAJI Mario Balotelli anajikuta katika wakati mgumu tena kwenye maiaha yake ya soka, baada ya kuitwa nyani mdogo na kaka wa mmiliki wa AC Milan, Silvio Berlusconi.
    Bosi wa gazeti, Paolo Berlusconi, mwenye umri wa miaka 64, alifanya ishara ya kushitusha dhidi ya Balotelli, mwenye umri wa miaka 22, kiasi cha saa kadhaa kabla ya mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City kuichezea mechi yake ya kwanza AC Milan kufuatia kurejea Italia.
    Berlusconi alikuwa amehudhuria mbio za FabrizioSala, mgombea mwenza wa kaka yake katika chama cha People of Freedom, wakati alipotoa maneno hayo na kupokedwa kwa kicheko na watu.
    Baada ya kutoa maneno ya utani kwa Nahodha wa Costa Concordia, Francesco Schettino, Berlusconi akamgeukia mshambuliaji Balotelli na kusema: 'Nimekwisha. Sasa tupo na toto kutoka familia ya manyani. Ni kichaa. Mabinti wote wanakaribishwa sana - unaweza pia kupata nafasi ya kuonana na rais (Silvio Berlusconi).'
    Dream debut: Balotelli netted twice on his AC Milan debut
    Balotelli alifunga mabao mawili katika mechi hiyo ya kwanza kuichezea AC Milan
    Dream debut: Balotelli netted twice on his AC Milan debut
    Paolo Berlusconi, ambaye pia ni Makamu wa rais wa AC Milan, pia ni Mhariri wa gazeti la Giornale, ambalo kaka yake amekuwa akilitumia sana kwa mambo yake ya kisiasa ya chama chake, People of Freedom na ndugu yake huyo amekwishahusishwa na kashfa kibao za rushwa.
    International duty: Balotelli is currently away with the Italy squad
    Balotelli kwa sasa yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Italia

     


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MWENYE TIMU AMUITA BALOTELLI NYANI AC MILAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top