Kocha wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall |
AZAM FC ilipanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2007/2008 na leo inacheza na Yanga SC kwa mara ya 10 tangu ipande katika ligi hiyo na kuleta changamoto kubwa katika soka ya Tanzania.
Katika mechi tisa za awali, Azam imeshinda tatu, imefungwa nne na kutoa sare mbili.
Katika mechi zote hizo, Azam imetikisa nyavu za Yanga mara 11, wakati zake zimetikiswa mara 13, huo ukiwa ni wastani wa kukusanya pointi 11, dhidi ya 14 za wapinzani wao hao.
Katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu, Yanga ilishinda mabao 2-0, leo timu hizo zinarudiana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, je Azam italipa kisasi na kufanya pia idadi ya mechi za kufungana na wana Jangwani hao iwe sawa nne kwa nne?
Bila shaka hilo na jambo la kusubiri na kuona, ila mchezo huo utakuwa mkali na wa kusisimua.
MSIMAMO WA MATOKEO YA MECHI
ZA YANGA NA AZAM:
P W D L GF GA Pts
Yanga SC 9 4 2 3 13 11 14
Azam FC 9 3 2 4 11 13 11
REKODI YA YANGA NA AZAM:
Oktoba 15, 2007
Yanga SC 3-1 Azam FC
Aprili 8, 2008
Azam FC 3-2 Yanga SC
Oktoba 17, 2009
Azam 1-1 Yanga SC
Machi 7, 2010
Yanga SC 2-1 Azam FC
Oktoba 24, 2010
Yanga SC 0-0 Azam FC
Machi 30, 2011
Yanga SC 2-1 Azam FC
Septemba 18, 2011
Azam 1-0 Yanga SC
Machi 10, 2012
Azam FC 3-1 Yanga SC
Novemba 4, 2012
Yanga SC 2-0 Azam FC