KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini anatarajia kupokea habari njema za kurejea uwanjani kwa beki wake, Micah Richards aliyekuwa majeruhi.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 24 yuko kwenye hatua za mwishoni za kurejea uwanjani tangu aumie goti Oktoba mwaka jana.
Richards anachosubiri ni ruhusa tu kutoka kwa mtaalamu wa masuala hayo, Andy Williams lakini City inajiamini itakuwa na beki huyo kwenye mazoezi kamili ndani ya wiki mbili hizi na anaweza akacheza mechi dhidi ya Aston Villa, Machi 4.
MIcah alipoumia