MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi jana ameiongoza Barcelona kutoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Granada katika La Liga na kufikisha mabao 301 aliyoifungia klabu hiyo.
Messi alifunga bao la kusawazisha dakika ya 50 na akafunga kwa mpira wa adhabu dakika ya 73 bao la ushindi, hilo likiwa bao lake la 37 katika msimu huu wa ligi.
Dakika ya mwisho kabisa, ki[a wa Granada, Tono aliokoa mchomo wa ana kwa ana na Messi na kumkosesha Hat-trick.
Messi akiifungia Barcelona bao la kwanza, ambalo lilikuwa la 300 tangu aanze kuvaa jezi ya Barca
Barca iliifuata Granada bila Xavi na David Villa na ikawaanzishia benchi Andres Iniesta, Jordi Alba na Carles Puyol.
Wenyeji wamezinduka katika La Liga chini ya kocha mpya, Lucas Alcaraz, wakishinda mechi mbili za kwanza bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa kabla ya mechi ya jana.
Granada iliifunga Real 1-0 wiki mbili zilizopita, siku ambayo Cristiano Ronaldo alijifunga, na ikaifunga Deportivo La Coruna 3-0 katika mechi iliyopita.
Messi akishangilia kufunga bao la ushindi jana
Mshambuliaji Odion Ighalo aliwafungia bao la kuongoza dakika ya 26 ambalo lilidumu hadi mapumziko, Messi a;lipowatibulia ushindi wa tatu mfululizo.