KLABU ya Manchester City imemuongeza katika orodha ya wachezaji inayowataka, beki wa Porto, Eliaquim Mangala mwishoni mwa msimu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, amekuwa akifuatiliwa na Manchester United, Bayern Munich na AC Milan katika miezi ya karibuni baada ya kuonyesha soka maridadi, ambayo iliivutia pia Arsenal.
Porto inataka Pauni Milioni 17.5 kwa kinda huyo wa kikosi cha Ufaransa cha vijana chini ya umri wa miaka 21 na itamuuza mwishoni mwa msimu.
Eliaquim Mangala (kulia) anafuatiliwa na Manchester City