DIDIER Drogba anatarajia kukutana
tena na rafiki zake wa zamani. Miezi tisa tangu afunge penalti ya ushindi pale Munich,
amerudi tena kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, akiwa na matumaini ya kufanya
maajabu mengine kwenye klabu yake mpya ya Galatasaray dhidi ya Schalke.
Mchango wake mkubwa wakati wa
harakati za Chelsea kutawala Ulaya, zilifikia keleleni Allianz Arena Mei mwaka
jana, pale alipofunga bao la kusawazisha katika dakika ya 88 na kukosa penalty
iliyookolewa katika muda wa nyongeza kabla ya kufunga penalty ya mwisho
iliyoamua bingwa.
Didier Drogba alianza maisha yake ya soka Galatasaray kwa kasi akifunga bao dakika ya tano tu ya mechi yake ya kwanza.
JE, DROGBA ATAFANYA VIZURI?
Muafrika wa Kwanza kufunga mabao 100, Ligi Kuu ya England
Mchezaji pekee kufunga kwenye fainali nne za Kombe la FA
Mfungaji Bora wa Kombe la UEFA, 2003-4
Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya England 2007, 2010
Timu Bora ya UEFA, 2007
Timu Bora ya FIFA/FIFPRO, 2007
Aliisaidia Chelsea kushinda Mataji yao mawili mfululizo ya kwanza
Aliiongoza Ivory Coast kushiriki Kombe la Dunia kwa Mara ya kwanza mwaka 2006 nchini Ujerumani.
Alifunga bao la kwanza la Ivory Coast kwenye Kombe la Dunia
Mchezaji Bora wa Afrika, 2006, 2009
Baada ya kuchukua Ubingwa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Drogba aliongea na Kombe, akiliuliza kwa nini limekuwa likimkwepa kwa muda mrefu, Jambo ambalo liliwashangaza wengi. “Lilikuwa kama tukio la Kidini,” alisema Mwenyekiti wa Chelsea, Bruce Buck.
Ujio wa Drogba Istanbul lilikuwa tukio ambalo liliwavuta wengi.
Maelfu ya watu waliajaza Uwanja wa ndege wakilitaja Jina lake, wakiwasha mafataki, mamia waliujaza uwanja wa mazoezi kumuangalia siku ya kwanza akifanya mazoezi.
Usajili wake ulikuwa wa pili wa mchezaji mwenye jina kubwa ndani ya mwezi mmoja katika klabu hiyo akifuata nyayo za Wesley Sneijder aliyetua kwenye klabu hiyo kwa ada ya pauni milioni 7, akitokea Inter Milan, Mholanzi huyo anaangalia uwezekano wa kufuata nyayo za Gheorghe Hagi katika klabu ya Galatasaray.
Lakini alikuwa ni Drogba ambaye alianza kwa kasi kwenye klabu hiyo akifunga bao la kichwa wakati timu hiyo iliposhinda kwa mabao 2-1 dhiodi ya Akhisar Belediye, alifunga bao hilo ikiwa ni dakika tano tu tangu aingie uwanjani akitokea benchi kucheza mechi yake ya kwanza.
Goli: Drogba akiifungia Chelsea bao la kusawazisha jijini, Munich Mei mwaka jana.
Ushindi: Drogba pia alifunga penalti ya ushindi na kuipa Chelsea Ubingwa wa Ulaya.
Kamaliza: Drogba akiwa na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Chelsea kushinda fainali dhidi ya Bayern Munich
MASHINE YA MABAO YA CHELSEA
Drogba alifunga mabao 157, katika mechi 341 alizoichezea klabu hiyo na kumfanya kuwa mfungaji bora wa nne wa muda wote wa klabu hiyo.
Mabao yake 34 kwenye michuano ya Ulaya ni Rekodi ya klabu kwa mabao 10.
Amefunga mabao tisa kwenye mechi tisa za fainali.
“Ni changamoto mpya, sehemu mpya ya maisha yangu,” alisema Drogba. Aliwaambia marafiki zake kwamba baada ya kuamua kuhama Shanghai Shenhua ya China chaguo lake la kwanza ilikuwa kuchezea klabu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa Drogba, (34), lilikuwa swali la kuutumia vizuri mwaka wake wa mwisho kama mchezaji. FIFA walimuunga mkono kuhama licha ya viongozi wa Shanghai, Kugoma. Wiki iliyopita alipewa Leseni ya kuchezea Galatasaray na Kamati ya Hadhi ya Wachezaji ya FIFA, wakati akisubiri kumalizika kwa utata wa mkataba wake.
Wakati Drogba akijiandaa kusikia kelele za mashabiki watakaokuwepo kwenye uwanja wa Turk Telekom Arena, wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 50,000, uwanja ambao umechukua nafasi ya ule wa Ali Sami Yen ambao pia ulikuwa na kelele kibao, atakuwa akijaribu kuongeza mabao kati ya yale 39 aliyonayo sasa kati ya mechi 77 za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Schalke, wanatakiwa kuwa na tahadhari. Lolote linaweza kutokea wakati Drogba na washikaji zake wa zamani wanapokuwa pamoja kwenye mechi za Ulaya.
Mashabiki: Drogba anatarajia mapokezi makubwa leo usiku.