// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KILA LA HERI SIMBA SC DHIDI YA LIBOLO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KILA LA HERI SIMBA SC DHIDI YA LIBOLO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 17, 2013

    KILA LA HERI SIMBA SC DHIDI YA LIBOLO

    Amri Kiemba, kiungo anayetarajiwa kuibeba Simba SC leo

    Na Mahmoud Zubeiry
    SIMBA SC leo inaanza kampeni yake michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikimenyana na Recreativo de Lobolo ya Angola katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mchezo huo, unatarajiwa kuwa mgumu, kutokana na Libolo ilivyoonekana kupania kupata matokeo mazuri kuanzia ugenini, ikiwasili mapema kwa zaidi ya wiki nzima mjini Dar es Salaam kuzoea hali ya hapa.
    Libolo imekuja Dar es Salaam ikitokea moja kwa moja Ureno, ilipokwenda kuweka kambi ya kujiandaa na michuano hii.
    Ilipowasili Dar es Salaam, imejilipia yenyewe hoteli, Double Tree, Masaki na Uwanja wa mazoezi, Gymkhana katikati ya Jiji.
    Maana yake Libolo ilituma watu wake mapema kuandaa mazingira ya ujio wao hapa. Pamoja na yote, Simba inajivunia rekodi yake nzuri katika michuano ya Afrika na leo wana matumaini ya kuwasimamisha Waangola hao Taifa.
    Katika mchezo wa leo, Simba itawakosa wachezaji wake wawili muhimu, beki Paul Ngalema ambaye amekuwa akicheza beki ya kushoto mwaka huu na mshambuliaji Mzambia, Felix Sunzu ambao ni majeruhi.
    Habari njema Amir Maftaha amerejea kikosini na amekuwa mazoezini na wenzake kwa zaidi ya wiki moja sasa, ingawa leo kushoto anaweza kuanzishwa Shomary Kapombe na kulia ‘dogo’ Miraj Adam.
    Juma Nyosso pia, aliyekuwa anatumikia adhabu ya kufanya mazoezi na kikosi cha pili, amerejea kikosi cha kwanza na anaonekana yuko fiti na haitakuwa ajabu leo akianza pamoja na Komabil Keita.
    Safu ya ulinzi itakamilishwa na mlinda mlango, Nahodha Juma Kaseja, wakati viungo wanaweza kuwa Amri Kiemba, Mussa Mudde, Mwinyi Kazimoto na Haroun Chanongo na washambuliaji wanaweza kuwa Mrisho Ngassa na Haruna Moshi ‘Boban’. 
    Simba imeshiriki kwa mafanikio misimu miwili iliyopita ya michuano ya Afrika, kwamba pamoja na kutofanikiwa kuingia hatua ya makundi, lakini mwishowe imekuwa ikifanya biashara nzuri ya kuuza wachezaji.
    Mwaka juzi iliwauza Mganda Patrick Ochan na mzalendo Mbwana Samatta klabu ya TP Mazembe ya DRC na Mussa Mgosi DC Motema ya nchini humo pia, wakati mwaka huu, ikiwa ni matunda ya ushiriki wao mwaka jana, imemuuza Mganda Emanuel Okwi Etoile du Sahel ya Tunisia.  
    Pamoja na kwamba imeanza kwa kusuasua mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara, ikizidi kuliweka rehani taji lake la ubingwa wa Ligi Kuu, lakini bado Simba inapoingia kwenye micuhuano ya Afrika inakuwa suala lingine.
    Mara ya mwisho Simba kukutana na timu kutoka Angola, ilikuwa ni mwaka 1993 katika Nusu Fainali ya Kombe la CAF, ambalo sasa limeunganishwa na Kombe la Washindi na kuwa Kombe la Shirikisho, ilipomenyana na AS Aviacao na kuitoa kwa jumla ya mabao 3-1, ikishinda 3-1 Dar es Salaam na kutoa sare ya 0-0 Angola.
    Hadi sasa kocha Mfaransa, Patrick Liewig aliyerithi mikoba ya Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick amekwishaiongoza Simba SC katika mechi 10, kati ya hizo ameshidna tatu tu, amefungwa tatu na kutoa sare nne.
    Lakini Liewig ni kocha mwenye historia nzuri katika michuano ya Afrika tangu akiwa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, ambayo anatarajiwa kuiendeleza Simba SC. Kila la heri Wekundu wa Msimbazi. 

    REKODI YA PATRICK LIEWIG SIMBA SC
    1. Simba SC 4-2 Jamhuri      (Kombe la Mapinduzi)
    2. Simba SC 1-1 Tusker FC  (Kombe la Mapinduzi)
    3. Simba SC 1-1 Bandari      (Kombe la Mapinduzi)
    4. Simba SC 0-1 U23 Oman  (Kirafiki)
    5. Simba SC 1-3 Qaboos      (Kirafiki)
    6. Simba 2-1 Ahly Sidab       (Kirafiki)
    7. Simba 0-1 Black Leopard  (Kirafiki)
    8. Simba 3-1 African Lyon     (Ligi Kuu)
    9. Simba SC 1-1 JKT Ruvu    (Ligi Kuu)
    10. Simba 1-1 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KILA LA HERI SIMBA SC DHIDI YA LIBOLO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top