// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HILI LI PICHA AMBALO MTAYARISHAJI MKUU LEODEGAR CHILLAH TENGA, TUSUBIRI TUONE MWISHO WAKE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HILI LI PICHA AMBALO MTAYARISHAJI MKUU LEODEGAR CHILLAH TENGA, TUSUBIRI TUONE MWISHO WAKE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, February 17, 2013

    HILI LI PICHA AMBALO MTAYARISHAJI MKUU LEODEGAR CHILLAH TENGA, TUSUBIRI TUONE MWISHO WAKE

    Na Bin Zubeiry

    NIMEMSIKILIZA kwa makini jana, rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), anayemaliza muda wake, Leodegar Chillah Tenga katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Kwa ufupi, kinachoendelea kwa sasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa TFF, inaonekana kama ni mchezo ambao umepangwa na dhamira maalum.
    Na si dhamira nyingine, watu wanalindana. Wanatengenezeana mazingira. Hii inanirudisha nyuma kidogo kwenye uchaguzi wa Yanga, uliomuweka madarakani Lloyd Nchunga- ulipangwa mchezo mkali sana na ukafanikiwa.
    Katika Mkutano wa jana, Tenga alianza kwa kutilia mkazo uamuzi wa Kamati ya Rufaa ya TFF kumuengua mgombea urais, anayepewa nafasi kubwa ya kushinda, Jamal Malinzi, akisema uamuzi huo ni sahihi na upo ndani ya taratibu, lazima uheshimiwe.
    Hata aliposema wanamruhusu kwenda Mahakama ya Usuluhishi (CAS), akasema; “Wakipeleka FIFA, FIFA wana taratibu hizo, lazima waje watuulize, jamani eeh, kuna nini huko. Sisi jibu letu litakuwa very simple, si mmepokea eeeh, njooni. Mkiweza njooni. Muulize, hatuna tabu, hilo ndilo jibu letu”. Maana yake watu hawa wamejipanga kuhakikisha Malinzi haingii kwenye uchaguzi na hata hao FIFA wakija, watapambana nao.
    Waandishi wa Habari walipomuuliza kuhusu, Malinzi iweje leo aonekane hafai, wakati mwaka 2008 alisimama naye kwenye uchaguzi wa shirikisho hilo, bado alionekana kujenga hoja za kuhalalisha uamuzi huo.
    Alidai eti, inawezekana walipopitia vema wasifu wake na kuunganisha muda aliotumikia vyombo mbalimbali vya michezo, haukufika miaka mitano. Eti labda umepungua hata mwezi mmoja.
    Bado alipoulizwa kuhusu maana ya uzoefu na kupitishwa kwa wagombea wengine ambao hawana uzoefu wa miaka mitano, akaendelea kujibu ‘kisiasa’.
    Hapa inachezwa rafu ya makusudi, ili kumbeba mtu. Hakuna anayeweza kusema nani anafaa kwa sasa kati ya mgombea Urais pekee aliyepitishwa kwa sasa, Athumani Jumanne Nyamlani na Malinzi anayefanyiwa mizengwe, lakini mtu makini yeyote lazima atasistiza haki.
    Katiba. Ni neno linalotumika vibaya mno na viongozi wa TFF.  Ni vigumu mno mtu kuihifadhi Katiba nzima ya TFF kichwani mwake, kiasi kwamba akiulizwa tu kuhusu kipengele chochote cha Katiba basi awe na jibu.
    Naamini, hata Tenga mwenyewe hajahifadhi Katiba nzima kichwani mwake, lakini kwa kuwa wanakaa nayo na wanaitumia kila wakitaka, basi wanaitumia vibaya.
    Bado kuhusu ujanja ujanja uliotumika kupitisha Katiba mpya, Tenga alikuja na majibu ambayo yaliwaacha Waandishi wanacheka tu. Hapa ndipo TFF ya Tenga inapopoteza sifa ya utawala bora.
    Tenga amekuwa hodari sana wa kuzungumza na ana maarifa ya kuteka hisia za watu, hasa sisi Waandishi wa Habari, ilipofikia anatumudu    
    Pamoja na viongozi wa serikali, wadau mbalimbali kuonekana kukerwa na hili la Malinzi kuenguliwa kiasi cha kupigia kelele, lakini mbele ya TFF ya Tenga ni sawa na kumpigia mbuzi gita. Watu wana dhamira yao, tena inaonekana ya muda mrefu na sasa inatekelezwa tu.
    Watu wanaiangalia kijuu juu FIFA, lakini ndani ya FIFA nako kuna mtandao maalum. Sepp Blatter ana mtandao wake naye ambao, ulimlinda katika uchaguzi wa FIFA na bila shaka naye anaulinda katika chaguzi zao, ili familia isisambaratike.
    Huo ndio upuuzi uliopo katika mpira wa miguu wakati mwingine, ni taasisi ambayo chini ya Blatter imejitengenezea mazingira fulani, unaweza kuyaita ya kidikteta.
    FIFA inasema serikali haziwezi kuingilia mambo ya mpira, lakini siku zote inasistiza serikali zisaidie mchezo huo. Fainali zipi za Kombe la Dunia zinaweza kufanyika popote duniani bila mkono wa serikali?
    Lakini viongozi wa FA waibe fedha, wafanye ubadhirifu wa fedha zilizotolewa na serikali na isifanye lolote, kisa? FIFA hairuhusu na ukifanya hivyo mtafungiwa.
    FIFA inalinda watu wake, na ilimlinda sana Muhiddin Ahmad Ndolanga wakati wake hadi akaishinda serikali na kujiita Tyson na sasa haitakuwa ajabu ikimlinda Tenga afanikishe anayoyataka, kumrithisha TFF mtu amtakaye.
    Kuna mambo mengi sana unayoweza kufikiria juu ya mchezo huo, kikubwa ni woga wa mabadiliko, visasi na kudhalilishana.
    Kwa mfano hivi sasa, pamoja na Tenga kusifia mara kwa mara mfumo wa utawala bora ndani ya TFF na uadilifu, lakini kuna kashfa nyingi kuhusu fedha, uadilifu na utawala bora, mambo ambayo bila shaka kiongozi yeyote mpya akiingia pale ataanza nayo.
    Rais Benjamin Mkapa amekuwa rais wa kwanza nchi hii kupanda kizimbani, ni jambo ambalo halipendezi kwa kiongozi mstaafu wa nchi.
    Ndolanga, Ismail Aden Rage na Michael Wambura wote walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za ubadhirifu baada ya kuondoka TFF, lakini kwa Tenga kama ataingia kiongozi swahiba wake pale, hatafanya hivyo hata kama kuna sababu.  
    Mpira ni jambo la hiari tu, lakini linalogusa hisia za wengi na wengi wanataka kujihusisha. Lakini si dhambi usipojihusisha, ila kwa sababu watu wanapenda kuwatumikia watu na mpira ni mchezo wa watu, ndio maana wanapenda.
    Na kwa sababu, kuna watu wameweka ngome, ili watu wengine wasiingie kuongoza mpira, tutafanya nini nao ndio wameshika msumeno kwenye makali? Jumapili njema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: HILI LI PICHA AMBALO MTAYARISHAJI MKUU LEODEGAR CHILLAH TENGA, TUSUBIRI TUONE MWISHO WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top