KIKOSI CHA KWNZA BRAZIL LEO;
Brazil: Julio Cesar; Daniel Alves, David Luiz (c), Dante, Adriano; Ramires, Paulinho; Oscar, Ronaldinho, Neymar; Luis Fabiano
KOCHA Roy Hodgson na vijana wake wanatambua ugumu watakaokutana nao kwenye mchezo wa leo usiku dhidi ya Brazil na tayari kocha wa wapinzani wake, Luiz Felipe Scolari amekwishataja kikosi cha kwanza.
Ronaldinho, Neymar na Luis Fabiano wanatarajiwa kuanza kwenye Uwanja wa Wembley, pamoja na nyota wa Chelsea, David Luiz, ambaye ni Nahodha wa kikosi hicho, Ramires na Oscar, na kipa wa Queens Park Rangers, Julio Cesar.
Neymar (kushoto) akimuangalia Ronaldinho (kulia)
Wengine wanaotarajiwa kuwamo kwenye kikosi hicho kitakachoivaa England ni pamoja na Daniel Alves, Dante, Adriano na Paulinho.
Nyota wa zamani wa Barcelona, Ronaldinho, mwenye umri wa miaka 32, mara ya mwisho aliichezea nchi yake mwaka uliopita ikifungwa 2-1 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Bosnia.
Hodgson tayari amethibitisha kwamba Steven Gerrard atakuwa Nahodha wa timu leo upande wa England, wakati Ashley Cole atacheza mechi ya 100 ya kimataifa.
Wachezaji wa Brazil mazoezini
Wachezaji wa Chelsea kikosini Brazil, Ramires, David Luiz na Oscar wote wanaanza leo