Nahodha wa Cameroon, Eto'o |
Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO
la Soka Cameroon (FECAFOOT) limetaja msafara wake wa watu 36 wakiwemo wachezaji
21 wa timu yao ya Taifa Indomitable Lions) wakiongozwa na Nahodha Samuel Eto’o
Fils kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumatano.
Kiongozi
wa msafara wa timu hiyo itakayoanza kuingia nchini keshokutwa (Februari 3 mwaka
huu) ni Mwakilishi wa Serikali ya Cameroon, Dieudone Wassi. Naibu kiongozi wa
msafara wa Cameroon itakayofikia hoteli ya New Africa ni Makamu wa Rais wa
FECAFOOT, John Ndeh.
Mbali
ya Et’oo, wachezaji wengine waliomo kwenye msafara huo ni Charles Itandje,
Benoit Assou Ekoto, Jehu Rustand Youthe (Union Douala), Fabrice Olinga Essono,
Allam Nyam, Bouba Aminou, Benoit Angwa, Herve Tchami, Henri Bedimo, Nicolas
Nkoulou, Jean Makoun, Jean Kana Biyick, Joel Matip, Vincent Aboubakar,
Alexandre Song, landre Nguemo, Pierre Wome, Jean Nyontcha, Achille Emana na
Charles Eloundou.
Wengine
ni Andre Nguidljol Nlend (Mkurugenzi wa Utawala FECAFOOT), Jean Paul Akono
(Kocha Mkuu), Martin Ndtouungou Mpile (Kocha Msaidizi), Jacque Songo’O (Kocha
wa makipa), Dk. Baoubakary Sidiki (Daktari wa Timu) na Emmanuel Francis Ambane
(Psychologist).
Pia
wapo Tchonkontey Monkam (Fitness Trainer), Rigobert Song (Meneja wa Timu),
Aoudou Mvotoung (Team Security), Fouda pascal Linus (Ofisa Habari FECAFOOT),
Boubakar Ndou (Meneja Vifaa), Daniel Tcheuffa Tecky (Physiotherapist), Elias
Kalaguem (Physiotherapist) na Justin Addo (Wakala wa Mechi).
Wakati
huo huo, kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
kitaingia kambini kesho jioni (Februari 2 mwaka huu) kwenye hoteli ya Tansoma.
Aidha,
kiingilio cha chini kwenye mechi ya FIFA Date kati ya Taifa Stars na Cameroon
itakayochezwa Jumatano (Februari 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kitakuwa ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani.
Viti
vya bluu ni sh. 7,000 wakati viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000. Kwa
viti vya VIP viingilio ni kama ifuatavyo; VIP C sh. 15,000, VIP B sh. 20,000 na
VIP A sh. 30,000.
Tiketi
zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo katika vituo vya Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohia/Samora,
kituo cha mafuta OilCom Ubungo, Dar Live Mbagala na kituo cha mafuta Buguruni.