DAVID Beckham alithibitisha kwamba miguu yake ya kizee bado iko fiti, na wakati Zlatan Ibrahimovic akiendeleza kasi yake ya kufunga wakati mastaa hao wawili walipoibeba Paris Saint-Germain, illipoilaza Marseille ya Joey Barton, kwa mabao 2-0 kufika robo fainali ya Kombe la Ufaransa.
Beckham alicheza kwa dakika 15 akitokea benchi, Jumapili wakati timu yake iliposhinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Marseille kwenye Ligi Kuu ya Ufaransa, na alitengeneza bao la pili la Ibrahimovic.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37, nahodha wa zamani wa England alicheza soka la hali ya juu huku akipewa kadi ya njano katika dakika za mwisho za mchezo huo, dakika chache kabla ya kutolewa uwanjani katika dakika ya 86 huku akishangiliwa na uwanja mzima wakati akitoka.
Kazi: Joey Barton akifanya shughuli kwa kumchapa David Beckham (kulia)
“Nimefurahi sana kucheza kwa dakika 86, nimefurahi sana,” Beckham alisema: “Nilijisikia poa. Nimekuwa nikifanya kazi kwa nguvu. Inanisadia kuwa na wachezaji wamenizunguka ambao wanafanya kazi kama hivi na kucheza kama hivi.”
Akicheza mbele ya mabeki wane, Beckham aliibeba kiungo ya PSG kwa pasi murua za kila wakati.
“Alikuwa na mchezo mzuri na ameonyeshja kwamba anaweza kudumu kwa muda mrefu,” alisema kocha wa PSG Carlo Ancelotti. “kuna vitu vingi ambavyo anaweza kutuonyesha – uzoefu wake, upigaji wake wa pasi, kujitoa kwake. Sidhani kama alicheza kama hana umri wa miaka 37.”
Ibrahimovic, kwa upande wake alionekana kutaka kumfunika kila mtu, wakati akifikisha mabao 26 kwenye michuano yote, alifunga bao lake la kwanza kwenye dakika ya 34, kabal ya kuongeza la pili kwenye dakika ya 64.
Mabao yake yamekuja masaa machache baaba ya Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) kutangaza kumfungia mechi mbili, hivyo atakosa mechi ijayo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, pia atakosa mechi yake ya kwanza ya robo fainali kama timu yake itasonga mbele.
Buti: Beckham (Kulia) akichapwa na kiungo wa Marseille, Jacques Romao
Beckham alimanusura azalishe bao kwenye dakika ya 62, baada ya Zoumana Camara kuunganisha kwa kichwa kona aliyopiga, lakini mpira uliokolewa kwenye mstari wa goli. Dakika chache baadaye alikaribia kuzichapa na mshambuliaji wa Marseille, Jordan Ayew baada ya dogo huyo kumchezea vibaya mara mbili. Baada ya tukio hilo waliendelea kubishana mpaka mwamuzi alipokuja kuwaamulizia.
“Mechi ilitawaliwa na ubabe kila kona, na ilikuwa kama hivyo kwenye mechi mwisho wa wiki, na itakuwa hivyo kwenye kila mechi kati ya PSG na Marseille,” Beckham alisema. “huwa unakumbuka matukio kama haya ukiwa nje ya uwanja, nilikutana na matukio kama haya nikiwa Marekani, ya leo ilikuwa poa sana.”
Beckham alipewa kadi ya njano na baadaye alitolewa nje na Ancelotti huku mashabiki wakiliimba jina lake “Dav-eed Beckham, Dav-eed Beckham,” pale Parc des Princes.
“Hatukutakiwa kusubiri mpaka usiku wa leo, kujua kuwa ni mpigaji pasi hodari na anajua sana kupiga mipira iliyokufa,” kocha wa Marseille, Elie Baup alisema.
Beckham alicheza chini sana mbele ya mabeki huku akiwa mezungukwa na Blaise Matuidi na Clement Chantome kila upande.

Angalia: Beckham aliisaidia timu yake kushinda mechi ya Kombe la Ufaransa
Dakika chache baada ya bao hilo wachezaji wa timu zote mbili walianza kuonyeshana ubabe kati kati ya uwanja baada ya Alaixys Romao kumchapa Beckham, Japokuwa hakuchukua hatua yoyote, kutokana na rafu hiyo na hata akafikia hatua kuamulia ugomvi pale mambo yalipoonekana kwenda kombo.
Beckham alijaribu kukaba mipira pale alipoweza lakini muda mwingi alikuwa akipata wakati mgumu kutoka kwa winga mwenye kasi Mathieu Valbuena ambaye mara kadhaa alimzidi kasi, hadi kufikia dakika ya 70 alionekana kuanza kuchoka kutokana na kuonekana akiwa ameshika mikono yake kiunoni huku akihema juu juu.
Lakini bado aliendelea kupambana hadi ikafikia wakati akapandishiana na Ayew, hata Joey Barton kuna wakati alionekana mara kadhaa akimvagaa Beckham, jambo ambalo lilisababisha viongozi wa timu zote mbili kuingilia ugomvi huo.
Bao: Zlatan Ibrahimovic akifunga bao la kwanza la PSG, chini akisherekea na wachezaji wenzake
“Nilipigwa kiwiko na Joey (Barton). Alifafanua tukio hilo baada ya mechi,” Beckham alisema. “Joey anawafanyia kazi nzuri na ni mchezaji mwenye kipaji. Namtakia kila la kheri.”
Dakika chache kabla ya hapo, UEFA walisema kwamba kamati yake ya nidhamu imemuongezea adhabu ya mechi mbili Ibrahimovic, kutokana na kumchezea vibaya Kiungo wa Valencia, Andres Guardado kwenye dakika za mwisho za mechi ya 16 bora mwanzoni mwa mwezi huu.
KWISHA: Ibrahimovic akipiga msumari wa mwisho kwenye jeneza la PSG kwa njia ya penalti