MSHAMBULIAJI Mario Balotelli ameendeleza mvua ya mabao katika klabu yake mpya, AC Milan ya Italia baada ya kufunga bao lake la nne katika mechi za tatu za ligi jana, likiwa ni bao moja zaidi kutoka yale aliyofunga katika nusu ya kwanza ya msimu 2012-13 klabu yake ya zamani, Manchester City.
Mshambuliaji wa Kitaliano, amekuwa moto mkali tangu arejee Milan na alifunga bao hilo kwa mpira wa adhabu dakika ya 78 kwenye Uwanja wa San Siro, timu yake ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Parma.
'Demu' wake, Fanny Robert Neguesha, mwanamitindo wa Kibelgiji, alikuwa jukwaani kumshuhudia 'laazizi' wake akipiga mpira wa adhabu kitaalamu.
Mario Balotelli akipiga shuti la mpira wa adhabu kufunga bao la ushindi kwa Milan dakika ya 78 dhidi ya Parma
Akishangilia bao lake
Kwa nini wakati wote mimi? Balotelli akishangilia bao lake San Siro
Balotelli akipongezwa na wachezaji wenzake, aliyekumbatiana naye ni Riccardo Montolivo
Tangu Balotelli aondoke Etihad Januari, mambo yamekuwa yakienda ovyo Manchester City ikitoa sare na QPR na Liverpool kabla ya kupigwa na Southampton na kupoteza matumaini ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu England.
Lakini mshambuliaji huyo 'Mtata', mambo yake yanamuendea vizuri, akianza na moto mkali katika klabu yake mpya, Milan.
Jukwaani na demu wa Balotelli, Fanny Robert Neguesha akionyesha ishara ya moyo, baada ya Balotelli kufunga bao, kuashiria anampenda mchizi wake