MSHAMBULIAJI Mario Balotelli aifanyiwa hila za kibaguzi na mashabiki wa Inter Milan wakati alipokabiliana na klabu yake hiyo zamani kwa kuonyeshwa ndizi.
Shahidi ambaye hakutaka kutajwa, aliionyesha Sportsmail video ambayo mashabiki fulani wa Inter waliinua ndizi kumuonyesha mshambuliaji huyo wa AC Milan katika mechi hiyo.
Licha ya kejeli hizo za kibaguzi, Balotelli alikuwa mtulivu na kuendelea kucheza na kuwajibu kwa kuweka kidole mdomoni mwake.
Balotelli akibishana na na mchezaji wa Inter, Javier Zanetti
Mashabiki wakionyesha ndizi kumkejeli Balotelli Uwanja wa San Siro