MSHAMBULIAJI Mario Balotelli usiku wa leo amefunga tena bao akiichezea klabu yake mpya, AC Milan akiinusuru kuzama mbele ya Cagliari kwa kupata sare ya 1-1 kutokana na bao lake la penalti.
Akitoka kufunga mabao mawili, likiwemo la penalti ya dakika ya mwisho Milan ikiifunga Udinese katika mechi yake ya kwanza kwenye klabu hiyo, siku saba zilizopita, mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 19, Januari kutoka Manchester City aliibeba tena timu yake mpya.
Mario Balotelli akifunga kwa penalti
Balotelli akishangilia bao lake na pia alifunga lingine ambalo lilikataliwa
Balotelli kazini