KLABU ya Arsenal imetolewa katika Kombe la FA baada ya kufungwa na Blackburn 1-0 katika mchezo wa Raundi ya Tano Uwanja wa Emirates leo.
The Gunners ambayo itapambana na Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne, leo iliwapumzisha wachezaji nyota kama Jack Wilshere, Theo Walcott na Santi Cazorla ambao kocha Arsene Wenger aliwaanzishia benchi kabla ya kuwaingiza baadaye.
VIKOSI VYA LEO
Arsenal: Szczesny, Vermaelen, Koscielny, Monreal, Diaby, Rosicky (Wilshere 70), Arteta, Oxlade-Chamberlain (Cazorla 70), Coquelin, Giroud, Gervinho (Walcott 70)
Benchi: Mannone, Sagna, Ramsey, Podolski
Kadi ya Njano: Coquelin
Blackburn: Kean, Orr, Martin Olsson, Dann, G Hanley, Lowe, Pedersen, Marcus Olsson (Bentley 63), Williamson, Rhodes (Goodwillie 83), Kazim-Richards
Benchi: Usai, Givet, Rekik, Nunes, Nuno Gomes
Kadi ya njano: Orr, Goodwillie
Mfungaji wa bao: Kazim-Richards dk72
Refa: Mike Dean
Mahudhurio: 60,070
Colin Kazim-Richards akiifungia Blackburn Rovers Uwanja wa Emirates
Gervinho akisikitika baada ya kukosa bao la wazi
Mikel Arteta akipiga mpira wa adhabu
Olivier Giroud (kulia) akikabiliana na mchezaji wa Blackburn, Jason Lowe (kushoto) kugombea mpira
Jack Wilshere (kushoto), Theo Walcott (katikati) na Santi Cazorla (kulia) wote waliingia kutokea benchi
Kipa wa Blackburn, Jake Kean leo alikuwa kikwazo kwa Arsenal
Alex Oxlade-Chamberlain (kulia) akijaribu kumtoka Grant Hanley (kushoto)
Tomas Rosicky alirejea kwenye safu ya kiungo ya The Gunners leo
Theo Walcott hoi
Kazim-Richards akishangilia mbele ya mashabiki wa Arsenal
David Bentley (kulia) aliichezea kwa mara ya kwanza Blackburn iliyomchukua kwa mkopo dhidi ya klabu yake ya zamani
Refa Msaidizi, maarufu kama mshika kibendera, Sian Massey akikagua nyavu kabla ya mechi