KLABU ya Arsenal imeungana na Tottenham na Juventus kumfuatilia beki wa kulia wa Sochaux, Sebastien Corchia, mwenye umri wa miaka 22.
Arsenal inafukuzia wachezaji tofauti, wakiwemo Daryl Janmaat wa Feyenoord, ambaye wanataka akarithi mikoba ya Bacary Sagna anayetarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu.
Sagna na klabu hiyo kwa sasa wapo kwenye majadiliano ya mkataba, na beki huyo Mfaransa amekataa kusaini miezi 12 ya nyngeza ya mkataba wake ambao utamfanya adumu hadi 2015.
Sebastien Corchia amezivutia Arsenal na Tottenham
Mkataba huo haujahusisha kuongezewa mshahara, maana yake ataendelea kulipwa pauni 60,000 kwa wiki.
Sagna aliumia mguu msimu uliopita na ameendelea kulalamika maumivu ya goti katika miezi ya karibuni.