KLABU ya Arsenal imefufua mpango wa kumsajili kiungo Mkenya wa Celtic ya Scotland, Victor Wanyama jana.
Ofisa msaka vipaji mwandamizi wa Gunners alikwenda Parkhead kushuhudia mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus ili kumtazama vizuri Mkenya huyo.
Vyanzo kutoka Arsenal vimesema kiwango cha Wanyama jana dhidi ya vigogo hao wa Serie A kinawaacgia kazi Arsene Wenger na Skauti wake Mkuu, Steve Rowley kuamua kumsajili au kutomsajili kiungo huyo baab kubwa.
Arsenal ilimtuma skauti wake mkuu kwenda Parkhead kumuangalia Victor Wanyama akicheza dhidi ya Juventus hapa
Wanyama alikuwemo kwenye kikosi kilichonyukwa 3-0 jana
Wenger ataingia sokoni kusaka kiungo mkabaji mwishoni mwa msimu, baada ya kumkosa nyota wa Toulouse, Etienne Capoue katika siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili la dirisha dogo.
Mbali na Wanyama na Capoue, kiungo wa West Ham, Momo Diame naye amekuwa akimulikwa kwenye rada za The Gunners.