ARSENAL wanataka kuweka sanamu la Dennis Bergkamp nje ya uwanja wake, wakati wa majira ya joto, hii ikiwa alama ya gwiji mwingine wa timu hiyo.
Sportmail limeona picha zinazoonyesha jinsi sanamu hilo litakavyo kuwa linafanana – litakuwa kwenye muundo kama wa kwenye picha ambayo alipigwa akimiliki mpira mwaka 2003 kwenye pambano dhidi ya Newcastle.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Uholanzi atashuhudia sanamu lake liliwekwa pembani ya sanamu la Thierry Henry, Tony Adams na Herbert Chapman ambayo yaliwekwa Disemba mwaka jana.
VIDEO: Angalia mabao bora ya Bergkamp akiwa na jezi ya Arsenal...
Mwana wa Dhahabu: Sanamu hilo litafanana na picha hii ya Dennis Bergkamp akimiliki mpira dhidi ya Newcastle
Kwa nini ni Gwiji wa Arsenal...
Mataji matatu ya Ligi Kuu ya England
Mataji manne ya Kombe la FA
Mabao 87, kwenye mechi 315
Bergkamp alikuwa kipenzi cha mashabiki wa the Gunners wakati akiwa na klabu hiyo kwa miaka 11
Baada ya kusajiliwa na Bruce Rioch kutoka Inter Milan kwa ada ya pauni milioni 7.5 mwaka 1995, aliiongoza Arsenal kwenye kilele chake cha mafanikio na kuchukua mataji.
Mshambuliaji huyo aliisaidia Arsenal kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu ya England – alikuwa kwenye kikosi kilichocheza mechi 49 za ligi kuu bila kufungwa mwaka 2004 – pia alishinda mataji manne ya Kombe la FA.
Mtaalamu wa Kiholanzi: Bergkamp akifunga bao lake la 87 akiwa na Arsenal
Akili ya ushindi: Bergkamp (wapili kushoto) akishangilia taji la FA mwaka 2005- lilikuwa taji la mwisho la Arsenal
Alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa PFA na Waandishi wa Habari za michezo mwaka 1998.
Msemaji wa Arsenal alisema: “Tuna masanamu matatu nje ya uwanja wa Emirates kwa ajili ya kumbukumbu ya magwiji wa Arsenal - Herbert Chapman, Tony Adams na Thierry Henry na tunashukuru kwamba yamekuwa yakiwavutia sana wanaotembelea uwanja huu.
Kazini: Bergkamp kwa sasa ni kocha msadizi wa Ajax akifanya kazi chini ya Frank De Boer
“Tunafurahishwa na uvumi uliozagaa juu ya sanamu letu linalokuja hapa Emirates, watu wanavutiwa na taarifa hizi na tutatangaza kila kitu juu ya maendeleo ya sanamu hilo.”
Bergkamp sasa hivi anafanya kazi kama msaidizi wa Frank de Boer katika klabu ya Ajax, baada ya kujifunza kazi hiyo kwenye klabu hiyo iliyomkuza.
Wakati huu ambao Arsene Wenger – ambaye alimfundisha Bergkamp Arsenal kwenye miaka ya nyuma akiwa kwenye wakati mgumu ndani ya Emirates, watu wamekuwa wakitamanio kumona Mholanzi huyo akirejea klabuni hapo kama kocha.
Wakati Liam Brady akiachia ngazi kama kocha wa chuo cha soka cha klabu hiyo, Bergkamp anatajwa kurithi jukumu hilo, lakini mwenyewe angependa kazi ya ukocha kamili wa klabu hiyo.
Gwiji Namba 1: Thierry Henry alitoa machozi pale Arsenal alipoona sanamu lake kwa mara ya kwanza Disemba 2011
Gwiji No 2 na 3: Herbert Chapman (kushoto) na Tony Adams pia wanamasanamu yao
Gwiji wa Magwiji: Staili ya ushanguliaji ya Tony Adams dhidi ya Everton ilitumika kwenye sanamu lake
VIDEO: Mabao matano bora ya Bergkamp Arsenal...
Siyo ajabu kuona Dennis Bergkamp akipata sanamu ndani ya Arsenal, hasa ukifikiria ubora wa magoli yake.
5: Arsenal v Southampton - Septemba 23, 1995
Bao la kwanza la Bergkamp akiwa na jezi za Arsenal halikuwa baya kwa kuanza nalo. Akiwa ametua kutoka Inter kwa ada iliyoweka rekodi ya klabu ya pauni milioni 7.5, watau walikuwa wakitarajia makubwa kutoka kwake, hakufunga kwenye mechi zake nane za kwanza, lakini mabao yake mawili dhidi ya Southampton yalikuwa ishara tosha ya kila anachoweza kukifanya. Alifunga kwa shuti kali la moja kwa moja katika dakika ya 17 ya mchezo akimalizia krosi ya Glenn Helder shuti ambalo lilimshinda Dave Beasant. Jinsi alivyouotea mpira huo ilikuwa nzuri sana, kipindi cha pili alifunga bao lake la pili kwa shuti kali la umbali wa yadi 25.
No 4: Arsenal v Bayer Leverkusen - Februari 27, 2002
Bao lake la nne kwenye ushindi wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya miamba ya Ujerumani, baada ya timu kutengeneza mashambulizi kutokea kwa Sylvain Wiltord ambaye alimpasia Bergkamp akiwa kwenye mstari wa goli, alichukua mpira huo kama anaenda pembeni na kumuangalia kipa akiwa ametoka nje kidogo ya lango kabla ya kuubetua mpira na kumpita Hans-Jorg Butt.
No 3: Arsenal v Bolton - Mei 5, 1996
Wakiwa wanahitaji kushinda ilikupata nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Arsenal walionekana kukaribia kupata sare, kabla ya Bergkamp kuchukua majukumu hayo begani kwake pale alipopokea pasi nzuri ya David Platt akiwa mita 25 nje ya goli, aligeuka kwa kasi ya ajabu na kuupiga mpira kwenda kwenye kona ya goli na kumshinda Keith Branagan na kuipa timu yake ushindi.
No 2: Newcastle v Arsenal - Februari 3, 2002
Ni bao ambalo alifanya kitendo ambacho, watu mpaka leo wanajiuliza alimaanisha kufanya ivo au aliotea tu. Lakini huyu ni Dennis Bergkamp. Ni lazima alimaanisha alichokifanya. Alijitengenezea nafasi nje ya eneo la hatari na kuomba mpira ambao alipasiwa na Robert Pires. Pasi ile ilipigwa nyuma yake lakini kwa kasi kubwa aliugusa mpira ule na mguu wake wa kushoto na kuzunguka akimpita Nikos Dabizas, na kumzidi nguvu beki mwingine kabla ya kukutana na mpira kwa mbele na kumfunga Shay Given kwa kutumia mguu wa kulia.
No 1: Leicester v Arsenal - Agostio 27, 1997
Hii ni moja kati ya hat-trick bora kwenye historia. Wakiwa na faida ya mabao mawili tayari, Bergkamp alifunga bao la tatu kwenye dakika ya 90, akimalizia kazi ya David Platt akiwa ndani ya eneo la hatari aliumiliki mpira na mguu wake wa kulia kabla ya kutumia mguu wa kushoto kuvuta ndani mpira kumkwepa Matt Elliott. Hakushughulika na beki huyo hata pale alipovutwa shati kabla ya kuipiga shuti lililomshinda Kasey Keller. Mholanzi huyo analitaja hili kama bao lake bora zaidi.