KOCHA wa Newcastle, Alan Pardew amelalamika kunyimwa mabao halali mawili yaliyofungwa na Papiss Cisse kwa madai eti alikuwa ameotea katika mchezo wa hatua ya 32 Bora ya Europa League na Metalist Kharkiv.
Pardew anashawishika kusema marefa wameidhulumu Newcastle ushindi halali na sasa watalazimika kusafiri hadi Ukraine timu zikiwa hazijafungana kupigania ushindi.
'Mabao yote yalikuwa halali,' alisema. '"Cha kusikitisha marefa wameyakataa mabapo yote, katika mchezo mgumu kama ule,"alilalamika Pardew.
Papiss Cisse akifunga bao lake la pili jana
Cisse alikuwa ana uhakika na bao lake hadi akaanza kushangilia
Kocha Pardew jana, hakuwa na hamu na marefa