MCHEZAJI Mholanzi, Nathan Ake wa Chelsea mwenye dreadlocks anaonekana kuwa na mwonekano wa Ruud Gullit.
Unamkumbuka? Gwiji wa Chelsea enzi hizo Ruud Gullit (kulia) unaweza ukamkumbuka kwa haraka ukimuona Nathan Ake (kushoto)
Ake akifanya mazoezi kuelekea mechi ya Chelsea ya Europa League mjini Prague na (chini) Ruud Gullit enzi zake
Beki huyo mwenye umri wa miaka 17 aliingia kuchukua nafasi ya Juan Mata katika mechi ambayo Chelsea ilishinda 1-0 ugenini dhidi ya Norwich na ingawa hakuwa na muda wa kutosha kuonyesha vitu vyake, lakini ilitosha kuonyesha dalili ni nyota anayechipukia.
'Kocha Rafael Benitez alinipa dakika chache na kuniambia nifurahie. Baada ya hapo, wachezaji walinipongeza, ilikuwa nzuri sana,' alisema Ake.
'Kweli nimefurahi sana, nina furaha na kujivunia, lakini kwa wakati huo huo, nakiri natakiwa kuendelea kujituma. Huu ni mwanzo tu.'
IAke aliichezea Chelsea kwa mara ya kwanza akitokea benchi kuchukua nafasi ya Juan Mata
Yumo kwenye kikosi cha Chelsea cha Europa League kitakachomenyana na Sparta Prague leo na amekuwa mchezaji wa kawaida kwenye benchi kwa wiki kadhaa sasa.
Chelsea ilimsajili kutoka Akademi ya Feyenoord mwaka 2010 (akifuata nyayo za Jeffrey Bruma) na ni soka yake baab kubwa iliyompa nafasi hiyo.
VIDEO: Angalia vitu vya Ake