Na Princess Asia
KAMPUNI
ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa shule yetuimeendelea
kutoa mchango wake katika sekta ya elimu ili kuboreshaelimu,
kuongeza idadi na ufaulu wa wanafunzi wa sayansi na kupunguza uhaba
wa vifaa vya kusomea mashuleni.
Airtel imefanya hivyo kwa kutoa msaada
wa vitabu vya kufundishia katika shule 3 za sekondari zilizoko Mkoani
Kagera mwishoni mwa wiki hii.
Shule
zilizofaidika na msaada wa vitabu hivi ni pamoja na shule za sekondari
za Kanyeranyere iliyoko muleba, Kirushya wilayani Ngara pamoja
na Nyamigogo iliyoko Biharamuro kagera Akiongea
wakati wa halfa fupi ya kukabidhi vitabu vya masomo ya sayansi
na hisabati Afisa elimu wa shule za sekondari mkoani Kagera Florian
Kimolo alisema" shule nyingi za sekondari katika mkoa wa Kagera
zimekuwa na upungufu mkubwa wa vifaa vya kujifunzia na
kufundishia
sanjari na uhaba wa vifaa vya maabara na walimu.
Kutokana na
upungufu wa vitendea kazi katika shule mbalimbali za sekondari hapa nchini
tunaomba wadau wa elimu kujitokeza katika kusaidia kulitatua tatizo
hilo ili shule hizo ziweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Tunashukuru
sana Airtel kwa mchango wao katika elimu na katika kuhakikisha
tunapata wanafunzi wengi wa masomo ya sayansi na walimu wanapata
vitabu vya kutosha katika kufundishia masomo haya na mwisho kupata
ufaulu wa kiwango cha juu.
Naye
Meneja mauzo wa Airtel katika mikoa ya Kagera na Kigoma Peter Kimaro
alisema " Airtel imejipanga kuendeleza ushirikiano na serikali ili
kuisaidia wizara ya elimu kufikia malengo waliojiwekea ikiwemo upatikanaji
wa vitabu mashule na kuongeza kiwango cha ufaulu.
Hadi sasa
kwa kupitia mradi wa " shule yetu tumeweza kufikia shule nyingi za
sekondari nchini. Na nimatumaini yetu vitabu tunavyowakabidhi leo vitaleta
mabadiliko ya elimu kwa shule hizi na mkoa wa Kagera kwa ujumla.
Naye
mkuu wa shule ya sekondari Kanyeranyere iliyoko wilyani Muleba mkoani
Kagera alitoa shukurani kwa niaba ya walimu wakuu wa shule za sekondari
za kanyeranyere, Kirushya na Nyamigogo na kusema, tunashukuru
Airtel kwa kuzikumbuka shule za mkoani Kagera, tunaahidi kuvitumia
vizuri vitabu hivi ili kuleta ufanisi zaidi na maendeleo ya
kitaaluma
katika shule zetu.
Airtel
imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia vitabu mashuleni, zaidi
ya shule 900 za sekondari hapa nchini zimenufaika kupitia kampeni
ya mradi wa kampuni ya simu za mkononi Airtel ujulikanao "Airtel
shule yetu".