• HABARI MPYA

        Wednesday, January 16, 2013

        ZAHOR PAZI ATIMKIA AFRIKA KUSINI KUJARIBIWA

        Zahor Pazi

        Na Prince Akbar
        KIUNGO mshambuliaji wa mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC, Zahor Iddi Pazi ameondoka leo Alfajiri Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Blomomfontein Celtic ya nchini humo.
        Baba mzazi wa mchezaji huyo, ambaye Desemba ametolewa kwa mkopo katika klabu ya JKT Ruvu Pwani, ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba kijana wake huyo amepatiwa nafasi hiyo na klabu yake ya Azam.
        “Alipokuwa Kongo (DRC) na Azam kwenye Kombe la Hisani kuna wakala alivutiwa na kipaji chake akaomba apelekwe kufanya majaribio, basi wakati umefika ameondoka leo,”alisema.
        Zahor licha ya kuwa mchezaji mzuri amekuwa hana bahati ndani ya kikosi chs Azam tangu asajiliwe msimu uliopita.
        Mwanzoni mwa msimu, Zahor aliomba kwenda kucheza kwa mkopo Coastal Union ya Tanga, lakini uongozi wa klabu hiyo ukamkatalia kabla ya kumtoa kwa mkopo Desemba mwaka jana.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments
        Item Reviewed: ZAHOR PAZI ATIMKIA AFRIKA KUSINI KUJARIBIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry