Yanga SC |
Na Baraka Kizuguto,
Antalya
Timu ya
Young Africans Sports Club kesho
itashuka dimbani kucheza na timu ya Denizlispor FC ya ligi daraja la kwanza
nchini Uturuki katika mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu utakaofanyika katika
uwanja wa Selen Football -Kalimya Complex pembeni kidogo ya mji wa Antlaya.
Young
Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo
kama fursa ya kujipima nguvu na timu hiyo la Denizlispor FC ambayo imeshuka kutoka ligi kuu ya Uturuki
mwaka jana na hivi sasa inapamabana kurudi tena katika Ligi Kuu ya Uturuki.
Kocha Mkuu
wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kupata nafasi ya
kucheza na timu kubwa kama ya Denizlispor FC ambayo ina wachezaji wa kiwango
cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
Baada ya
kuwa na wiki moja ya mazoezi na mechi moja ya kirafiki dhidi ya Armini
Bielefeld ya ujerumani mwishoni mwa wiki itakua ni fursa nyingine nzuri ya
kucheza mchezo wa kirafiki na timu nyingine, hii itanisadia kuona maendeleo ya
kikosi changu kutokana na mazoezi ambayo tumekuwa tukiyafanya tangu tulipofika
alisema 'Brandts'
Denizlispor
FC ni miongoni mwa timu zaidi ya 200 kutoka shemu tofauti duniani ambazo
zimeweka kambi katika mji wa Antlaya kwa ajili ya maandilizi ya mzunguko wa
pili wa Ligi Daraja la kwanza nchini Uturuki.
Mchezaji wa
zamani wa Leicester City ya Uingereza, Dundee United ya Scotland na Ivernes ya
Uholanzi, mtanzania mzaliwa wa Uingereza Eric Odhiambo ni miongoni mwa
washambuliaji wa kutegemewa wa timu ya Denizlispor FC.
Young Africans
imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa
na mchezo huo utakaochezwa kesho katika uwanja wa Selen Football - Kalimya
complex pemebeni kidogo ya mji wa Antalya.
Kikosi cha
wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna
maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji
yoyote katika mchezo huo.
Athumani Idd
'Chuji' na Hamis Kiiza waliokuwa wakijisikia vibaya kabla ya mchezo wa juzi
dhidi ya Amrnini Bielefeld wanaendelea vizrui kabisa kwani wanaendelea na
mazoezi pamoja na wachezaji wengine waliopo na timu mjini Antalya.
Kuhusu hali
ya hewa leo haijaonekana kuwa tatizo kwa wachezaji kwani wanaonekana kuimudu na
mda mwingi kwa sasa kumekua na jua linalowaka kuanzia asubuhu wakati wa mazoezi
mpaka mida ya jioni, kwa leo hali ya hewa ni nyuzi joto 17 - 21, hivyo hali ya
hewa ni nzuri tu.